-
Ukosoaji wa Iran kwa namna Magharibi inavyolitumia kisiasa suala la haki za binadamu
Apr 07, 2025 03:40Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa hatua ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa dhidi yake na kueleza kwamba kulitumia kisiasa suala la haki za binadamu ni sababu muhimu ya kupoteza imani kwa taasisi hiyo na imesisitiza kuwa, nchi zinazouunga mkono utawala wa Kizayuni katika mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ghaza hazina ustahiki wa kutoa madai ya kutetea haki za binadamu.
-
Mkuu wa Wakala wa Nishati ya Atomiki wa UN: Iran haina silaha za nyuklia
Apr 06, 2025 03:04Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, amekariri madai ya kisiasa anayotoa kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa Tehran; na pamoja na kueleza kwamba ijapokuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina akiba kubwa ya urani iliyorutubishwa lakini haina silaha za atomiki, ametaka kuharakishwa mchakato wa kutatua masuala ya usimamizi wa mradi wake wa nyuklia.
-
Iran: Vitisho vya US vinakinzana na wito wake wa diplomasia
Apr 05, 2025 23:29Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekosoa lugha ya vitisho dhidi ya Tehran, akisisitiza kuwa nchi hii iko tayari kufanya mazungumzo lakini "katika mazingira ya usawa."
-
Rais wa Iran amfuta kazi Makamu wake kwa 'safari ya ubadhirifu'
Apr 05, 2025 06:07Rais Masoud Pezeshkian amempiga kalamu nyekundu Makamu wake katika Masuala ya Bunge kufuatia safari ya kibinafsi ya mwanasiasa huyo wakati wa sherehe za mwaka mpya wa Kiirani (Nowruz), iliyojaa ubadhirifu.
-
Kuwa tayari Iran kuimarisha ushirikiano na nchi za eneo
Apr 04, 2025 06:57Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na wakuu wa baadhi ya nchi za eneo na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi hizo katika nyanja mbalimbali kwa mujibu wa imani na itikadi za Kiislamu.
-
Pezeshkian: Mataifa ya Kiislamu yanaweza kukomesha jinai za Israel
Apr 03, 2025 08:08Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa ya Kiislamu unaweza kuwa chachu ya kukomeshwa jinai za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Iran yakosoa unafiki wa Wamagharibi kwa kufumbia macho jinai za Israel
Apr 03, 2025 03:37Iran imelaani vikali kuendelea kwa mashambulizi na jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan; hususan katika sikukuu za Idul-Fitri, na kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya ukiukaji wa haki zinazofanywa na utawala huo ghasibu.
-
Trump atafakari pendekezo la mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran
Apr 02, 2025 23:05Ikulu ya Marekani White House inatathmini pendekezo la kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran; na wakati huo huo inaongeza kiwango cha vikosi vya jeshi lake vamizi katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ili kujiandaa kwa operesheni tarajiwa za kijeshi dhidi ya Tehran.
-
"Saudia, UAE, Qatar, Kuwait zapiga marufuku ndege za US kufanya mashambulio"
Apr 02, 2025 23:04Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Uajemi yamepiga marufuku ndege za kivita za Marekani kutumia viwanja vyake vya ndege au anga zao kufanya mashambulizi dhidi ya Yemen.
-
Araghchi: Maadui watajuta kwa kutoa vitisho dhidi ya Iran
Apr 01, 2025 08:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitamruhusu mtu yeyote kuzungumza nayo kwa lugha ya ubabe na vitisho, akiwaonya maadui kwamba watajuta kulitishia taifa hili.