-
Iran yaonya: Shambulio dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia litasababisha 'vita vitakavyoenea katika eneo'
Jan 31, 2025 23:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ametoa onyo kali kuhusu matokeo mabaya ya kitendo cha uchokozi kinachoweza kufanywa, ambacho kinaweza kuuhusisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Spika wa Baraza la Hamas apongeza mchango wa Iran katika kuwatetea Wapalestina
Jan 31, 2025 23:03Muhammad Ismail Darwish, Mwenyekiti wa Shura ya Hamas, ametoa shukurani kwa msaada na uungaji mkono wa Iran kwa watu wa Palestina, na kusema mchango wa Tehran ni muhimu katika mapambano yanayoendelea dhidi ya utawala wa ghasibu wa Israel.
-
Iran yaanza sherehe za Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jan 31, 2025 10:03Raia wa Iran leo wameanza sherehe za Alfajiri Kumi ili kuadhimisha mwaka wa 46 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyouangusha utawala wa kifalme wa Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na kusaidiwa na Marekani.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Mafanikio muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na elimu
Jan 31, 2025 10:00Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu anakutambua kuzalisha elimu na sayansi kuwa ndio njia ya kupata nguvu na kuwa imara, na mafanikio yenye thamani kubwa zaidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni uzalishaji wa sayansi na harakati ya kuelekea kwenye kilele cha elimu inaofanywa na vijana mahiri wa Iran.
-
Pezeshkian: Iran haijapokea ujumbe wowote kutoka Marekani
Jan 29, 2025 07:40Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haijapokea ujumbe wowote kutoka Washington hadi sasa.
-
Uhusiano wa kibiashara wa Iran na Oman wazidi kustawi
Jan 29, 2025 00:06Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara wa Iran ametangaza habari ya kuzidi kustawi na kuimarika uhusiano wa kibiashara baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Oman.
-
Iran yasikitishwa na shambulio la droni lililoua 70 hospitalini Darfur, Sudan
Jan 27, 2025 08:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei amelaani shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya hospitali moja katika mji wa El Fasher katika mkoa wa magharibi wa Darfur nchini Sudan, na kusababisha vifo vya makumi ya watu.
-
Iran yakanusha tuhuma za Israel za kupeleka silaha Lebanon
Jan 25, 2025 08:05Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amepuuzilia mbali madai ya Israel kamba Jamhuri ya Kiislamu inasafirisha kimagendo silaha kwenda Lebanon.
-
Afkham: Azimio la Bunge la Ulaya dhidi ya Iran halina msingi wa kisheria
Jan 25, 2025 07:51Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu na Masuala ya Wanawake ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema azimio lililopasishwa hivi karibuni na Bunge la Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu halina msingi wowote wa kisheria na linaonyesha tabia ya uingiliaji ya chombo hicho.
-
Pezeshkian: Iran na Russia hazitakubali kuburuzwa na maadui
Jan 24, 2025 23:33Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa, mapatano kamili ya ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Russia yanaonyesha kwamba Tehran na Moscow kamwe hazitakubali matakwa ya kupindukia ya maadui, akisisitiza kuwa nchi mbili hizi zitashirikiana kuunda sera zinazotoa kipaumbele kwa masuala ya utulivu, usalama, maendeleo na ustawi wa uchumi katika eneo.