-
Axios: Netanyahu atasusiwa na sehemu kubwa ya wawakilishi wa Congress
Mar 22, 2024 03:29Tovuti ya habari ya Marekani ya Axios imesema kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, huenda akasusiwa pakubwa na "wabunge wa Congress ikiwa atakubali mwaliko wa kuzungumza mbele ya Bunge la Marekani.
-
UNICEF: Israel inaendesha "vita vya kuwalenga watoto" wa Ghaza iliyowekewa mzingiro
Mar 21, 2024 23:00Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF James Elder amesema matukio yanayojiri katika Ukanda wa Ghaza ni "vita dhidi ya watoto," na kusisitiza kuwa eneo hilo hivi sasa si mahala pa kuishi watoto.
-
Utafiti: Aghalabu ya Wasaudia wanapinga uhusiano wa Waarabu na Israel
Mar 21, 2024 07:34Uchunguzi mpya wa maoni unaonyesha kuwa, akthari ya wananchi wa Saudi Arabia si tu wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, bali pia wanataka nchi zote za Kiarabu zivunje mahusiano yao na utawala wa Kizayuni.
-
Ukosoaji wa Afrika Kusini dhidi ya Israel kwa kukaidi uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Mar 21, 2024 04:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa kutotekelezwa maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya Israel kunaidhoofisha mahakama hiyo.
-
Muqawama wa Iraq washambulia uwanja wa ndege Tel Aviv
Mar 20, 2024 23:23Kwa mara nyingine tena wanamuqawama wa Iraq wameshambulia Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, Tel Aviv.
-
Israel: Tumeua watu 90 katika Hospitali ya al-Shifa
Mar 20, 2024 22:41Jeshi la utawala haramu wa Israel limekiri na kutangaza wazi kuwa askari wake wameua Wapalestina 90 katika uvamizi na hujuma ya siku mbili katika Hospitali ya al-Shifa huko katika Ukanda wa Gaza.
-
Misri: Operesheni ya kijeshi ya Israel huko Rafah itakuwa na matokeo mabaya
Mar 18, 2024 23:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema Marekani inapasa kuileza wazi Israel kuhusu taathira hasi na matokeo mabaya ya utawala wa Kizayuni kuushambulia kijeshi mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS: Muqawama wa kupambana na Israel umevuka mipaka ya Ghaza
Mar 18, 2024 07:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema utawala wa Kizayuni wa Israel unakabiliwa na "safu pana zaidi" ya Muqawama iliyovuka mpaka wa Ukanda wa Ghaza.
-
HRW: Magharibi inaendelea kuipatia Israel silaha wakati inajadili kupeleka misaada Ghaza
Mar 18, 2024 07:43Wakati wabunge katika nchi nyingi za Magharibi wanajadili ni kwa kiwango gani utawala wa Kizayuni wa Israel unaweza ukawa unakwamisha upitishaji misaada ya kuokoa maisha ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza, mauzo ya silaha ambayo yanachangia vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala huo dhidi ya eneo hilo lililowekewa mzingiro yangali yanaendelea kumiminika.
-
Mkuu wa WHO aiambia Israel: 'Kwa jina la ubinadamu' futeni mpango wa kuivamia kijeshi Rafah
Mar 17, 2024 02:26Shirika la Afya Duniani (WHO) limeutaka kwa msisitizo mkubwa utawala wa Kizayuni wa Israel uchukue uamuzi wa kufuta mpango wake wa kuuvamia na kuushambulia kijeshi kupitia ardhini mji wa Rafah ulioko kusini ya Ukanda wa Ghaza, unaohimili vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala huo.