Utafiti: Aghalabu ya Wasaudia wanapinga uhusiano wa Waarabu na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109746-utafiti_aghalabu_ya_wasaudia_wanapinga_uhusiano_wa_waarabu_na_israel
Uchunguzi mpya wa maoni unaonyesha kuwa, akthari ya wananchi wa Saudi Arabia si tu wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, bali pia wanataka nchi zote za Kiarabu zivunje mahusiano yao na utawala wa Kizayuni.
(last modified 2024-03-21T07:34:34+00:00 )
Mar 21, 2024 07:34 UTC
  • Utafiti: Aghalabu ya Wasaudia wanapinga uhusiano wa Waarabu na Israel

Uchunguzi mpya wa maoni unaonyesha kuwa, akthari ya wananchi wa Saudi Arabia si tu wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, bali pia wanataka nchi zote za Kiarabu zivunje mahusiano yao na utawala wa Kizayuni.

Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na taasisi ya utafiti ya 'Center for Internal Security Studies' umebainisha kuwa, asilimia 96 ya watu walioshirikishwa kwenye utafiti huo wanasisitiza kuwa, Waarabu hawapasi kuwa na uhusiano wowote na Israel, kutokana na jinai za kutisha zinazofanywa na utawala huo pandikizi huko Gaza.

Maandamano ya kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika mataifa ya Kiarabu, na yalishtadi baada ya Wazayuni kuanza kufanya mauaji ya kimbari huko Gaza Oktoba 7, 2023.

Utafiti wa 'Center for Internal Security Studies' umefichua kuwa, hata kabla ya kuanza vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza, asilimia 87 ya Wasaudia walikuwa wanaitakidi kuwa utawala wa Kizayuni utashindwa, na Wapalestina wataibuka washindi.

Maandamano ya Wakuwait ya kupinga uhusiano na Israel

Uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa karibuni na taasisi ya 'The Washington Institute for Near East Policy' ulionyesha kuwa, asilimia 96 ya Wasaudia wanapinga mpango wa Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni baada ya vita vya Gaza.

Kadhalika washiriki wa uchunguzi huo wa maoni wamesisitiza kuwa, nchi za Kiarabu zinapaswa kukata kabisa uhusiano na utawala ghasibu wa Israel kwa ajili ya kulalamikia hujuma na jinai za Wazayuni huko Gaza.