-
Wataalamu wa UN: Kuipelekea silaha Israel kukomeshwe mara moja!
Feb 24, 2024 23:05Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limeonya kwamba upelekaji wowote wa silaha au risasi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo zitatumika katika mashambulizi ya ardhini na angani dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghazza uliozingirwa unaweza ukawa unakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, na lazima ukomeshwe mara moja.
-
Idhini mpya ya Uingereza kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya umati dhidi ya wananchi wa Palestina
Feb 23, 2024 04:57Uingereza ambayo ni moja ya waungaji mkono wakuu wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina sambamba na Ujerumani na Marekani, hivi sasa imetoa idhini mpya kwa Israel ya kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina hasa wa Ghazza. Madola hayo matatu ya Magharibi ndiyo yaliyoko mstari wa mbele katika kuusheheneza silaha hatari utawala wa Kizayuni ili uzidi kuua raia wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Rais wa Brazil afananisha jinai za Israel na zile za Hitler wa Ujerumani
Feb 21, 2024 23:09Jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza zinahesabiwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo ya karibuni na aghalabu ya jinai hizo zimetajwa kuwa ni maangamizi ya kizazi huku zikilinganishwa na uhalifu ulizofanywa na Adolf Hitler, kiongozi Manazi wa Ujerumani, katika Vita vya Pili vya Dunia.
-
Afrika Kusini yaiasa ICJ iseme ukaliaji wa ardhi za Palestina ni kinyume cha sheria
Feb 20, 2024 09:24Afrika Kusini imeiomba Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itoe ushauri wa kisheria unaosema kuwa hatua ya Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina ni kinyume cha sheria.
-
Brazil yamuita nyumbani balozi wake wa Israel, mzozo watokota
Feb 20, 2024 09:22Serikali ya Brazil imemrejesha nyumbani balozi wake wa Israel, huku mzozo wa kidiplomasia ukiendelea kutokota baina ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini na Tel Aviv.
-
Iran: Kuipatia Israel dola bilioni 14 ni sawa na Marekani kutoa bakhshishi kwa mauaji ya Wapalestina
Feb 19, 2024 07:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuidhinishwa na Baraza la Seneti la Marekani msaada wa dola bilioni 14 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kunaonyesha kuwa Washington inautuza na kuupa bakhshishi utawala huo kwa kuwaua kwa halaiki raia wasio na hatia wa Palestina katika vita visivyo na mlingano vya Gaza.
-
ICJ yaanza kusikiliza shauri la kihistoria kuhusu uhalali wa Israel kukalia ardhi za Palestina kwa miaka 57
Feb 19, 2024 07:40Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ambayo ndiyo mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa leo imeanza kusikiliza shauri la kihistoria la kuamua kuhusu uhalali wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wa kuzivamia na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina kwa muda wa miaka 57.
-
Anadolu yataja orodha ya silaha zilizofanyiwa majaribio na Israel katika vita vya Gaza
Feb 18, 2024 23:37Shirika la habari la Anadolu la Uturuki limeripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakabiliwa na kesi ya mashtaka ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ huko Hague Uholanzi umezifanyia majaribio silaha nyingi kwa mara ya kwanza katika mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7 mwaka jana.
-
Mashirika yaitaka AU isiipe Israel uanachama kwenye umoja huo
Feb 17, 2024 08:55Kundi moja la asasi za kiraia limeutaka Umoja wa Afrika utupilie mbali ombi la utawala wa Kizayuni wa Israel la kuwa mwanachama mtazamaji wa AU, na kufufua mjadala uliodumu kwa miaka miwili kuhusu kadhia hiyo.
-
Marekani kuitumia Israel mamia ya mabomu aina ya MK-82
Feb 17, 2024 08:04Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani inapanga kutuma shehena za mabomu na silaha nyingine zenye thamani ya makumi ya mamilioni ya dola kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kumwaga damu za Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.