-
Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: Hatutashiriki uchaguzi mkuu wa Desemba 28
Oct 09, 2025 10:37Upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umetangaza kuwa utasusia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Disemba ambapo Rais Faustin-Archange Touadera atawania tena urais kwa muhula wa tatu.
-
Uganda kutoa mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati
Sep 06, 2025 03:04Jeshi la Uganda UPDF litatoa mafunzo ya kijeshi ya muda wa miezi sita kwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Afrika Kati katika hatua ya kuisadia nchi hiyo kujenga upya jeshi lake baada ya miaka ya mingi ya kuvurugika kwa amani na utulivu nchini humo.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28
Aug 20, 2025 06:27Jamhuri ya Afrika ya Kati itaendesha uchaguzi mkuu Disemba 28 mwaka huu baada ya kuakhrishwa mara kadhaa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya jana Jumanne.
-
AU yaeleza kuridhishwa na usitishaji mapigano, kuvunjwa makundi yenye silaha Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jul 19, 2025 03:59Umoja wa Afrika, AU umeeleza kuridhishwa na usitishaji mapigano unaotekelezwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuvunjwa kwa makundi mawili ya wabeba silaha nchini humo, na unetoa wito kwa makundi mengine pia kukabidhi silaha zao.
-
Mahakama ya UN yatoa waranti wa kukamatwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
May 01, 2024 10:52Mahakama Maalumu ya Jinai (CPS) inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imesema, imetoa hati ya kukamatwa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi wakati wa uongozi wake.
-
Zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha baada ya boti kupinduka Jamhuri ya Afrika ya Kati
Apr 21, 2024 07:57Takriban watu 58 waliokuwa wakienda mazishini wameaga dunia baada ya boti yao kupinduka majini katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. Haya yalielezwa jana na mkuu wa ulinzi wa raia.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati yapinga azma ya Marekani ya kutuma silaha nchini humo
Dec 24, 2023 07:10Jamhuri ya Afrika ya Kati imelaani hatua ya Marekani ya kutaka kupeleka zana za kijeshi nchini humo.
-
Ukatili wa kingono CAR; UN kuwatimua askari 60 wa Tanzania
Jun 10, 2023 11:22Umoja wa Mataifa umesema utawafukuza makumi ya askari wa Tanzania, ambao ni sehemu ya Kikosi cha Kulinda Amani cha moja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) kwa kutuhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono.
-
Mahakama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yawahukumu kifungo wanamgambo 3 kwa jinai dhidi ya binadamu
Nov 02, 2022 02:47Mahakama Maalumu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imewapata na hatia wanamgambo watatu kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu na kuwahukumu vifungo vya jela kuanzia miaka 20 hadi vifungo vya maisha.
-
Mahakama Jamhuri ya Afrika ya Kati yaanza kusikiliza kesi ya kwanza ya jinai za kivita
May 17, 2022 07:36Mahakama Inayoendesha Kesi za Uhalifu wa Kivita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeanza kusikiliza kesi ya kwanza ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na jinai za kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Kikao cha kwanza cha Mahakama Kuu ya Uhalifu Afrika ya Kati kilifanyika kusikiliza kesi ya watuhumiwa wa uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.