Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129744-jamhuri_ya_afrika_ya_kati_kufanya_uchaguzi_mkuu_disemba_28
Jamhuri ya Afrika ya Kati itaendesha uchaguzi mkuu Disemba 28 mwaka huu baada ya kuakhrishwa mara kadhaa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya jana Jumanne.
(last modified 2025-08-20T06:27:12+00:00 )
Aug 20, 2025 06:27 UTC
  • Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28

Jamhuri ya Afrika ya Kati itaendesha uchaguzi mkuu Disemba 28 mwaka huu baada ya kuakhrishwa mara kadhaa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya jana Jumanne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne, Bruno Yapande, Waziri wa Masuala ya Utawala wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alieleza kuwa wapiga kura watamchagua Rais, wabunge, na wawakilishi wao wa mikoa na manispaa. 

Amesema, mchakato wa uchaguzi unakwenda kwa kasi licha ya kuwepo baadhi ya changamoto. 

Takriban wapiga kura milioni 2.3 wameajiandikisha kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba na orodha ya mwisho ya daftari la wapiga kura inatazamiwa kutolewa tarehe 29 mwezi huu wa Agosti. 

Rais Faustin Archange Touadera, aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016 kuiongoza Jamhuri ya Afrika ya Kati na akachaguliwa tena mwaka wa 2020 kuwa Rais, mwezi Julai alitangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu licha ya kukabiliwa na ukosoaji.

Licha ya kukosolewa, Rais Archange anasifiwa kwa kuboresha  hali ya usalama baada ya miaka mingi ya mizozo na machafuko.