-
Ukosoaji wa Mkuu wa Baraza Ulaya dhidi ya siasa za kuzusha mizozo za Rais Donald Trump
Aug 26, 2019 03:45Siasa na hatua za Rais Donald Trump wa Marekani katika nyanja mbalimbali hususan kuiondoa Washington katika mikataba na makubaliano ya kimataifa kama ya nyuklia ya JCPOA, mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris Ufaransa na vilevile hatua yake ya kung'ang'ania kuwa na vita vya kibiashara na madola mengine makubwa kiuchumi duniani, ni mambo ambayo yamepelekea kuibuka mizozo mikubwa katika uga wa kimataifa.
-
Mazungumzo ya viongozi wa Ufaransa na Marekani kuhusu Iran na JCPOA
Aug 25, 2019 08:21Mivutano iliyopo baina ya Marekani na nchi za Ulaya zilizomo katika kundi la 4+1 kuhusiana na jinsi ya kuamiliana na Iran na kadhia nzima ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA bado ni moja ya mivutano mikubwa ya pande hizo mbili. Katika wiki za hivi karibuni, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alifanya mazungumzo mbalimbali na marais wa Iran na Marekani na kuja na mapendekezo ya kupunguza wasiwasi uliopo.
-
Dakta Zarif: Madola ya Ulaya yatekeleze kivitendo ahadi zao za JCPOA
Aug 24, 2019 07:53Waziri wa Mashauri yay Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, endapo madola ya Ulaya yatatekeleza kivitendo ahadi zao za makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, basi Iran nayo iko tayari kuachana na hatua ilizochukua za kupunguza uwajibikaji wake kwa mujibu wa makubaliano hayo.
-
Sisitizo la Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na Ujerumani juu ya kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Aug 23, 2019 02:50Baada ya Marekani kujiondoa kinyamela katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) Mei mwaka jana, kinyume na matarajio ya Washington ambayo ilitaka nchi zingine wanachama wa kundi la 5+1 nazo zichukue uamuzi kama wake, mataifa hayo ikiwemo Russia na Ujerumani yalisisitiza juu ya kuendelea kubakishwa makubaliano hayo ya kimataifa yaliyokuwa yamepata baraka kamili za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Rouhani: Kujiondoa Marekani katika JCPOA kuna maana ya kukiuka makubaliano ya kimataifa na ugaidi wa kiuchumi
Aug 22, 2019 22:15Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kujiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kuna maana ya kuvunja mkataba, kukiuka ahadi, kupuuza makubaliano ya kimataifa na ugaidi wa kiuchumi.
-
Zarif: Nchi za Ulaya bado hazijatekeleza ahadi zao katika mapatano ya JCPOA
Aug 21, 2019 20:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kufungamna Iran na mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kusema: "Baada ya Mareakni kujiondoa katika mapatano haya, nchi za Ulaya hazijatekeleza ahadi zao."
-
Abbas Mousavi: Mazungumzo ya JCPOA kati ya Iran na Ulaya hayajafikia natija
Aug 19, 2019 03:44Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mwenendo wa mazungumzo ya Iran na madola ya Ulaya kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, mazungumzo kuhusiana na uwajibikaji wa Ulaya katika JCPOA hadi sasa hayajawa na natija.
-
Sisistizo la anayechukua nafasi ya Mogherini na Troika ya Ulaya kuhusu kulinda JCPOA
Aug 15, 2019 05:44Umoja wa Ulaya na Troika ya umoja huo yaani, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, kama wanachama wa kundi la 4+1 wamekuwa wakidai kuwa wanaunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA. Pamoja na hayo, hivi sasa Ulaya inakabiliwa na changamoto kubwa katika kulinda mapatano ya JCPOA. Ni kwa msingi huo ndio wakuu wa Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya wakasisitiza kuhusu kulinda JCPOA.
-
Rais Rouhani: Kudhamini usalama wa Ghuba ya Uajemi hakuhitajii vikosi vya kigeni
Aug 14, 2019 08:21Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ili kudhamini usalama na utulivu katika Ghuba ya Uajemi hakuna haja ya kuweko vikosi vya kieneo katika eneo hilo.
-
Jahangiri: Marekani inalenga kuvuruga usalama wa Ghuba ya Uajemi
Aug 13, 2019 02:43Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Eshaq Jahangiri amesema Marekani inalenga kuvuruga usalama wa Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la kistratijia la Hormuz na kutumia ukosefu wa usalama kama kisingizo cha kujiimarisha kijeshi katika eneo.