Zarif: Nchi za Ulaya bado hazijatekeleza ahadi zao katika mapatano ya JCPOA
(last modified Thu, 22 Aug 2019 01:12:56 GMT )
Aug 22, 2019 01:12 UTC
  • Zarif: Nchi za Ulaya bado hazijatekeleza ahadi zao katika mapatano ya JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kufungamna Iran na mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kusema: "Baada ya Mareakni kujiondoa katika mapatano haya, nchi za Ulaya hazijatekeleza ahadi zao."

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo Jumatano alipohutubu katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) nchini Sweden na huku akiashiria kuwa mapatano ya JCPOA yameweka utaratibu wa hatua za kuchukuliwa iwapo waliofikia mapatano hayo watayakiuka, ameongeza kuwa: "Marekani haiwezi haiwezi kutumia mapatano hayo kama chombo cha maslahi yake binafsi."

Halikadhalika ameashiria hatua ya tatu ambayo Iran itachukua katika kupunguza utekelezaji wa ahadi zake katika JCPOA baada ya pande zingine kukiuka ahadi zao na kusema: "Hatua hii itakuwa imara zaidi ya zilizotangulia."

Aidha ameashiria namna ambavyo Rais Donald Trump hawezi kutabirika na kusema:" Wakati unachukua hatua zisizoweza kutabirika, basi upande wa pili nao pia utachukua hatua zisizoweza kutabirika na katika hali hiyo kutakuwa na mvurugiko".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria kuwepo muungano wa kijeshi wa Marekani na Ulaya katika Ghuba ya Uajemi na kusema: "Wakati wanapoisimamisha meli ya mafuta ya Iran katika eneo la Jabal al Tariq (Gibraltar) na kuanzisha vita vya kiuchumi dhidi ya Iran, basi wafahamu kuwa hawawezi kuleta usalama katika Ghuba ya Uajemi."

Zarif ameendelea kusema kuwa, Iran ina mpaka wenye urefu wa kilomita 1,500 katika pwani ya Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman na hivyo hakuna jeshi lolote la majini linaloweza kudumisha amani katika eneo hilo.

Akiashiria hatua ya Saudi Arabia na baadhi ya nchi za eneo kununua idadi kubwa ya silaha, Zarif amesema usalama wa eneo hauwezi kununuliwa.

Tags