Feb 03, 2017 04:21
Umoja wa Mataifa umesema unatiwa wasiwasi na hali ya usalama ya raia wa Yemen katika miji ya Dhubab na Almakha iliyoko kwenye mkoa wa Taiz. Kuhusiana na suala hilo, Jamie McGoldrick, Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ametoa taarifa na kutangaza kuwa ripoti kutoka maeneo hayo zinaonyesha kwamba operesheni za kijeshi zilizofanywa kwenye maeneo ya pwani ya miji ya Dhubab na Almakha zimewafanya wakaazi wake walazimike kuzihama nyumba zao.