Wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio nambari 2234 la kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usimamishe ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, waziri wa vita wa utawala huo haramu ameafiki shauri la kujengwa ukuta wa uzio katika mipaka ya Ukanda wa Gaza.
Katika radiamali yake ya kwanza kabisa kuhusiana na mgogoro wa Syria katika kipindi cha katibu mkuu António Guterres, Umoja wa Mataifa umelaani kitendo cha magenge ya kigaidi cha kuwakatia maji wananchi wa Damascus Syria na kusema hiyo ni jinai ya kivita.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kwa mara nyingine limetoa wito kwa Marekani kusitisha uuzaji wake wa silaha kwa Saudi Arabia.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ametoa taarifa akiituhumu Marekani kwamba, imetenda jinai za kivita nchini Afghanistan.
Mahakama maalumu nchini Senegal imemhukumu kifungo cha maisha jela mtawala wa zamani wa kijeshi wa Chad, Hissene Habre baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na kutenda jinai dhidi ya binadamu, utesaji na utumwa wa ngono.
Wananchi wa mji mkuu wa Yemen, Sana'a wamefanya maonyesho ya picha, michoro na mabango yanayoakisi jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia dhidi ya raia wa Yemen
Ndege za kivita za Saudi Arabia Jumamosi zilidondosha mabomu katika soko moja lenye idadi kubwa ya watu katika mkoa wa Sana'a nchini Yemen.