-
Tume ya Kupambana na Ufisadi Kenya yazuia kuunganishwa Telkom na Airtel ili kuchunguza ufisadi
Aug 28, 2019 22:06Tume ya Kupambana na Ufisadi Kenya (EACC) imesema imesimamisha mpango wa kuunganishwa kampuni ya simu ya binafsi ya Airtel na ile ya Telkom, ambayo sehemu moja ya hisa yake inamilikiwa na serikali, ili kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha yanayodaiwa kufanywa katika kampuni ya Telkom.
-
Kusafirishwa shehena ya kwanza ya mafuta ya Kenya kwaibua madai ya mgao wa mapato
Aug 26, 2019 22:12Kenya imesafirisha kwa ajili ya kuuza nje ya nchi shehena yake ya kwanza ya mafuta ghafi jana Jumatatu, huku viongozi wa maeneo inakopatikana maliasili hiyo wakiitaka serikali itekeleze ahadi yake ya kugawa kwa haki na kama ilivyoafikiwa mapato yatakayopatikana katika shehena zijazo.
-
Kenya: Mgogoro wa mpaka wa baharini kati yetu na Somalia utatuliwe kwa mazungumzo
Jul 20, 2019 05:00Serikali ya Kenya inaendelea kusisitiza kuwa, nchi jirani ya Somalia inapaswa kuheshimu mamlaka ya ardhi ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki, huku Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ ikitazamiwa kutoa hukumu mwezi Septemba mwaka huu, juu ya mvutano wa mpaka wa baharini kati ya nchi mbili hizo.
-
Wakenya waendelea kujadili kauli ya Raphael Tuju kuwa Odinga alitumia suala la kujitenga, kumsuka Rais Kenyatta akubali handisheki
Jul 15, 2019 12:15Wananchi wa Kenya wameonyesha kushangazwa na kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, nchini Kenya, Raphael Tuju, aliyesema jana kuwa, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alitumia suala la kujitenga kwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa yakimuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2017, ili kumsukuma Rais Uhuru Kenyatta aweze kukubali kadhia ya handisheki.
-
Watanzania na Wakenya ni miongoni mwa 26 waliouawa katika shambulizi Somalia
Jul 13, 2019 08:14Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja kusini mwa Somalia imeongezeka na kufikia watu 26. Awali Polisi ya Kismayo iliripoti kuwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi ni watu saba.
-
Ripoti: Wakenya zaidi ya milioni 2 katika hatari ya kufa njaa
Jul 02, 2019 07:17Mamilioni ya Wakenya wapo katika hatari ya kukumbana na baa la njaa na mgogoro mkubwa wa chakula kuanzia mwezi huu wa Julai.
-
Mbunge 'Jaguar' anyimwa dhamana nchini Kenya + Sauti
Jun 28, 2019 12:43Mahakama nchini Kenya imemnyima dhamana, Mbunge wa eneobunge la Starehe jijini Nairobi Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ ambaye alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mbunge huyo atasalia korokoroni hadi pale kesi yake itakaposikilizwa tena. Mwandishi wetu wa Mombasa, Kenya Seifullah Murtadha ana maelezo zaidi......
-
Kamati ya Mshikamano wa Wakenya na Wapalestina: Muamala ya Karne utagonga mwamba
Jun 27, 2019 12:29Vuguvugu la mshikamano baina ya Wakenya na Wapelestina limekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Mbunge Jaguar wa Kenya aliyetaka kutimuliwa wafanyabiashara wa kigeni atiwa mbaroni
Jun 26, 2019 08:00Mbunge wa Jimbo la Starehe jijini Nairobi nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ amekamatwa leo na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
-
Mgonjwa mwenye dalili za Ebola Kenya awekwa karantini
Jun 17, 2019 08:01Mgonjwa anayeshukiwa kuwa na Ebola nchini Kenya amewekwa katika karantini katika Hospitali ya Kericho magharibi mwa nchi hiyo.