-
Iran yavunja rekodi katika uuzaji wa gesi ya LPG Afrika, Asia
Feb 10, 2018 13:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweka rekodi mpya katika uuzaji wa gesi aina ya LPG katika nchi kadhaa za mabara ya Afrika na Asia ambapo iliuza tani 520,000 Januari mwaka huu hilo likiwa ni ongezeko la asilimai 39.4 kutoka mwezi uliotangulia.
-
Polisi Kenya yamkamata mbunge wa tatu aliyeshiriki hafla ya kujiapisha Odinga
Feb 03, 2018 12:16Polisi ya Kenya imemtia nguvuni kwa muda na kumsaili mbunge wa tatu wa kambi ya upinzani nchini humo kwa tuhuma ya kushiriki katika hafla ya kuapishwa kinara wa kambi ya upinzani Raila Odinga kuwa "kiongozi wa wananchi" badala ya Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo aliyeshinda uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.
-
UN yaitaka serikali ya Kenya iheshimu uhuru wa vyombo vya habari
Feb 03, 2018 04:05Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Kenya kuheshimu agizo la mahakama lililoitaka ibatilishe hatua yake ya kuzifungia televisheni tatu kupeperushaji matangazo baada ya stesheni hizo kurusha moja kwa moja hafla ya kuapishwa kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Raila Odinga.
-
AU,EU wamkosoa kinara wa upinzani Kenya, Odinga, kwa kujiapisha
Feb 03, 2018 01:20Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini KenYa, Raila Odinga amelaaniwa vikali na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kwa kujiapisha kama 'rais wa wananchi' Januari 30 na kusema hatua hiyo inakiuka utawala wa sheria.
-
Serikali ya Kenya yapuuza amri ya Mahakama; yaendelea kukata matangazo ya stesheni tatu za TV
Feb 02, 2018 04:34Urushaji matangazo wa vituo vitatu vya televisheni nchini Kenya umeendelea kusimamishwa licha ya amri ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo kuiamuru serikali iondoe zuio hilo.
-
Mahakama Kuu ya Kenya yaagiza kufunguliwa kwa runinga zilizokatiwa matangazo
Feb 01, 2018 11:10Mahakama Kuu nchini Kenya imesimamisha agizo la serikali ya nchi hiyo la kufunga kwa muda usiojulikana urushaji wa matangazo ya vituo vitatu maarufu vya televisheni nchini humo.
-
SAUTI, Serikali ya Kenya yakosolewa na viongozi wa dini kwa hatua yake ya kuzifungia televisheni tatu nchini humo
Jan 31, 2018 15:31Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekosolewa na viongozi wa dini nchini humo kutokana na hatua yake ya kuzifungia televisheni tatu kupeperushaji matangazo baada ya televisheni hizo kurusha moja kwa moja hafla ya kuapishwa kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Raila Odinga.
-
Stesheni tatu za TV Kenya kuendelea kufungwa kwa kutangaza hafla ya kuapishwa Odinga
Jan 31, 2018 12:02Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya amesema vituo vitatu vya televisheni vitaendelea kufungwa kwa muda usiojulikana wakati serikali inachunguza hafla ya "kuapishwa" kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo Raila Odinga.
-
Odinga 'aapishwa' kuwa 'rais wa wananchi' Kenya, viongozi wenzake wasusa
Jan 30, 2018 13:21Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga 'ameapishwa' hii leo kuwa 'rais wa wananchi' katika sherehe ilizofanyika katika Bustani ya Uhuru jijini Nairobi.
-
Wasiwasi watanda Kenya huku Odinga akijiandaa kuapishwa kama 'rais'
Jan 30, 2018 04:38Wasiwasi umetanda nchini Kenya hii leo katika siku ambayo Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA Raila Odinga ametangaza kuwa ataapishwa kama 'rais' hatua ambayo serikali imesema ni uhaini na hukumu yake ni kunyongwa.