Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imekitaja kitendo cha Saudi Arabia cha kuwanyonga mateka kadhaa wa Yemen kuwa ni mfano wa wazi wa jinai ya kivita.
Shirika la ujasusi wa kijeshi la serikali ya mamluki wa Saudi Arabia inayoongozwa na rais mkimbizi Abdu Rabuh Mansour Hadi, limewahukumu kifo maafisa wake kadhaa kwa kushindwa kuulinda mkoa wa Maarib.
Mahakama ya Misri imetoa hukumu ya kifo kwa wapinzani 24 wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa dhidi ya rais halali wa zamani wa nchi hiyo marehemu Muhammad Morsi.
Fahd bin Turki bin Abdulaziz Aal Saud, kamanda wa ngazi za juu wa jeshi vamizi la Saudi Arabia nchini Yemen amehukumiwa kifo na Baraza la Kijeshi la Saudia kwa tuhuma za uhaini.
Idara ya Magereza ya Misri inayoongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo imetangaza kuwa, imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya watu 9 waliohukumiwa kwa hatia ya kile kinachotajwa kuwa ni uvamizi dhidi ya kituo cha polisi.
Jumuiya 16 za kimataifa zimemuandikia barua mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa bin Salman al-Khalifa zikimtaka azuie utekelezaji wa adhabu ya kifo dhidi ya vijana wawili kwa kosa la kuwashambulia polisi.
Tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini Marekani daima imekuwa na utendaji hasi na wa kihasama dhidi ya taifa hili la Kiislamu.
Mahakama moja nchini Misri imewahukumu adhabu ya kifo watu 37 akiwemo Hisham al Ashmawy afisa wa zamani wa jeshi la nchi hiyo aliyejiunga na magenge ya kigaidi.
Katika kipindi cha miezi 9 iliyopita ya mwaka huu wa 2019, Saudi Arabia imeshatekeleza adhabu ya kifo kwa watu 160 na kuvunja rekodi yake ya huko nyuma ya kutekeleza adhabu hiyo kwa watu wengi zaidi duniani.
Shirika la kupinga adhabu ya kifo limetangaza kuwa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umenyonga watu zaidi ya 130 katika mwaka huu, aghlabu yao wakiwa wapinzani wa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman.