Mahakama ya Jinai ya Cairo nchini Misri imewahukumu kifo watu 28 kati ya 67 wanaotuhumiwa kumuua aliyekuwa mwanasheria mkuu wa nchi hiyo.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekutaja kuua raia kuwa ni silaha ya kisiasa inayotumiwa na utawala wa Saudi Arabia kwa ajili ya kuwanyamazisha wapinzani wake.
Katika kuendelea ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia, utawala wa Aal Saud umewanyonga raia wanne wa nchi hiyo wa mji wa Qatif.
Viongozi wa kijeshi katika eneo la Puntland, kaskazini mwa Somalia, wamewanyonga wanachama saba wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la ash-Shabab.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema utawala wa Aal-Saud umepanga kuwanyonga wanaharakati 14 wa Kishia eti kwa kosa la kushiriki maandamano.
Mahakama moja nchini Saudi Arabia imewahukumu adhabu ya kifo wanaharakati 14 kwa kushiriki maandamano katika eneo la Qatif.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema Bahrain inaelekea kutumbukia katika mgogoro wa haki za binaadamu na inapaswa kusitisha mara moja hukumu ya kunyongwa wafungwa wengine wawili wa kisiasa nchini huo.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya utawala wa Aal-Khalifa wa Bahrain ya kuwanyonga wanaharakati watatu wa nchi hiyo kwa madai bandia ya kuhusika na shambulizi la kigaidi la mwaka 2014.
Mahakama maalumu ya Riyadh nchini Saudi Arabia imeendelea kutoa hukumu ya kifo dhidi ya wafungwa wa kisiasa kwa kuwakatia adhabu ya kifo watu 15 kwa tuhuma zisizo na msingi wowote eti za kufanya ujasusi kwa maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Umoja wa Mataifa umepongeza hatua ya Kenya ya kubadilisha adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha jela kwa maelfu ya watu waliokuwa wakisubiri kutekelezwa hukumu hiyo dhidi yao.