-
Wasiwasi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka uingiliaji wa kigeni nchini Libya
Jul 09, 2020 21:54Vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Libya vimechukua sura mpya na tata na hasa kufuatia uamuzi wa wapiganaji wanaojiita Jeshi la Kitaifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar wa kuanzisha hujuma ya kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, mnamo mwezi Aprili 2019 na uingiliaji wa nchi za kigeni kwa ajili ya kuziunga mkono pande hasimu katika mgogoro huo.
-
Guterres: Uingiliaji wa kigeni wa hivi sasa Libya haujawahi kushuhudiwa
Jul 09, 2020 10:55Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema uingiliaji wa madola ya kigeni katika mgogoro wa Libya unaoshuhudiwa hivi sasa upo katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tena huko nyuma.
-
Lavrov: Haftar yuko tayari kusaini makubaliano ya kusitisha vita nchini Libya
Jul 08, 2020 19:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa wanamgambo wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya wako tayari kusaini makubaliano ya kusitisha vita nchini humo.
-
GNA Libya yaapa kujibu mapigo kwa waliokishambulia kituo cha anga cha al-Watiya
Jul 06, 2020 06:49Naibu Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya (GNA) amesema, vikosi hivyo vitajibu mapigo katika wakati na mahali mwafaka kwa waliohusika na shambulio dhidi ya kituo cha anga cha al-Watiya.
-
Rais wa Ageria: Libya itakuwa Somalia mpya barani Afrika
Jul 05, 2020 04:49Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesema kuwa, hali inayoshuhudiwa sasa nchini Libya inafanana na ile ya Syria kutokana na nchi kadhaa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
-
Uturuki yasisitiza kushirikiana na Serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya
Jul 04, 2020 23:23Waziri wa Ulinzi wa Uturuki ameutembelea mji mkuu wa Libya Tripoli, na kusema nchi yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya (GNA).
-
Misri yawasiliana na mtoto wa Gaddafi ili kujinufaisha kiuchumi nchini Libya
Jul 04, 2020 07:20Baadhi ya duru za Misri zimesema kuwa, mashirika ya kijasusi ya nchi hiyo yamewasiliana na mwana wa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kwa ajili ya kumshinikiza kisiasa na kujinufaisha na fursa za kiuchumi nchini humo.
-
Uturuki: Ufaransa imefumbia macho jinai zinazofanywa na UAE, Misri nchini Libya
Jul 01, 2020 21:45Balozi wa Uturuki mjini Paris ameituhumu Ufaransa kuwa inaegemea upande mmoja na kwamba imefumbia macho jinai zinazofanywa na Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri nchini Libya.
-
Nchi za Sahel Afrika zaomba kufutiwa madeni yote kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi
Jul 01, 2020 06:52Mkutano wa nchi Sahel Afrika na Ufaransa umetoa wito wa kufutwa madeni yote ya nchi hizo ili kusaidia juhudi za kupambana na athari mbaya zilizosababishwa na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, mapambano dhidi ya ugaidi na mikakati ya ustawi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
-
Indhari ya Umoja wa Ulaya kuhusu kupuuzwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya
Jun 30, 2020 21:56Katika hali ambayo mgogoro wa Libya ungali unaendelea kutokota sambamba na uingiliaji wa madola mbalimbali katika masuala ya ndani ya nchi hiyo huku misaada ya kijeshi ya kisilaha ikiwa imeifanya hali ya nchi hiyo kuzidi kuwa mbaya, Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, vikwazo vya silaha dhidi ya Libya daima vimekuwa vikikiukwa na jambo hilo kufanyiwa mzaha.