-
Biden akariri madai yasiyo na msingi kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran
Apr 29, 2021 07:39Rais Joe Biden wa Marekani amekariri tena madai yake yasiyo na msingi kuhusiana na miradi ya kuzalisha niishati ya nyuklia nchini Iran.
-
Mazungumzo ya Vienna, maendeleo na changamoto zake
Apr 28, 2021 05:35Katika fremu ya utekelezaji wa hatua za kistratijia kwa ajili ya kufuta vikwazo vya kidhalimu na kulinda maslahi ya taifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilichukua hatua za kulipiza kisasi ikijibu hatua ya Marekani na kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile hatua ya nchi za Ulaya ya kutotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa makubaliano hayo.
-
Mawakili watajika duniani: Mauaji ya watu weusi yanayofanywa na Polisi wa Marekani ni jinai dhidi ya binadamu
Apr 28, 2021 03:34Mawakili watajika wa haki za binadamu duniani kote waliofanya uhakiki kuhusu ukatili unaofanywa na polisi ya Marekani wametangaza kuwa, mauaji na mashambulio ya kuwajeruhi raia weusi yanayofanywa na askari polisi wa nchi hiyo yamefikia kiwango cha jinai dhidi ya binadamu.
-
Katika siku 100 za kwanza za urais wake, Biden ametoa kauli 67 za uongo na upotoshaji
Apr 27, 2021 23:14Jopo la kutafiti uhakika wa mambo la gazeti la Washington Post limeeleza katika ripoti yake ya kutathmini siku 100 za kwanza za utendaji wa Rais Joe Biden wa Marekani, kwamba katika hotuba alizotoa, mahojiano aliyofanyiwa na jumbe za Twitter alizotuma hadi sasa, kiongozi huyo ametoa madai 67 ya uongo au upotoshaji mambo.
-
CAIR: Manyanyaso dhidi ya Waislamu yaliongezeka kwa asilimia 9 nchini Marekani mwaka uliopita
Apr 27, 2021 03:14Kundi linaloongoza kwa kutetezi haki za Waislamu nchini Marekani lilitangaza Jumatatu ya jana kwamba kumekuwepo ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka uliopita wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.
-
Kuanza mchakato wa kuondoka askari wa Marekani na wa NATO kutoka nchini Afghanistan
Apr 26, 2021 23:51Jenerali Austin Scott Miller, kamanda wa askari wa Marekani na wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) nchini Afghanistan alitangaza Jumapili iliyopita katika mkutano wake na waandishi wa habari kwamba, mchakato wa kuondoka wanajeshi wa Marekani na wa NATO huko Afghanistan umeanza katika baadhi ya vituo vya kijeshi nvya nchi hiyo na kwamba, vituo vyote vya kijeshi vitakabidhiwa kwa vikosi vya Kiafghani.
-
Saudi Leaks: Bin Salman anatumia pombe, ni mraibu wa dawa za kulevya
Apr 26, 2021 23:50Mtandao wa Saudi Leaks umefichua kuwa, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman anatumia dawa za kulevya ni ni mraibu wa heroni.
-
Wamarekani zaidi ya elfu 13 wameaga dunia kwa silaha moto tangu mwanzoni mwa mwaka huu
Apr 26, 2021 23:50Ripoti iliyotolewa katika makavazi ya ukatili wa silaha nchini Marekani inaonyesha kuwa, zaidi ya watu elfu 13 wamepoteza maisha katika matukio ya ufyatuaji risasi nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021.
-
Malalamiko yaendelea Marekani kupinga ubaguzi na ukandamizaji wa polisi
Apr 25, 2021 21:59Maandamano yanaendelea katika jimbo la Carolina Kaskazini nchini Marekani kulaani ubaguzi wa rangi na ukandamizaji wa jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kuuliwa na polisi, Mmarekani mwengine mwenye asili ya Afrika kwenye jimbo hilo.
-
Yafichuka: Bin Salman anahonga vyombo vya habari ili kusafisha sura yake duniani
Apr 25, 2021 07:49Mtandao mmoja wa habari nchini Marekani umefichua kuwa, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman amefunga mkataba wa gharama kubwa ya fedha na kampuni moja ya Marekani kwa shabaha ya kuboresha sura yake iliyochafuka sana mbele ya macho ya walimwengu.