Ujerumani yakamilisha mchakato wa kuondoa askari wake Afghanistan; US?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i71842-ujerumani_yakamilisha_mchakato_wa_kuondoa_askari_wake_afghanistan_us
Ujerumani imetangaza kuwa imemaliza mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake huko Afghanistan, huku Marekani ikiripotiwa kuwa inapanga kuwaacha mamia ya wanajeshi wake nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 30, 2021 11:10 UTC
  • Ujerumani yakamilisha mchakato wa kuondoa askari wake Afghanistan; US?

Ujerumani imetangaza kuwa imemaliza mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake huko Afghanistan, huku Marekani ikiripotiwa kuwa inapanga kuwaacha mamia ya wanajeshi wake nchini humo.

Akitoa tangazo hilo, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Annegret Kramp-Karrenbauer amesema: "Baada ya kutumwa (Afghanistan) kwa karibu miaka 20, wanajeshi wetu wa mwisho wa Bundeswehr wameondoka Afghanistan jioni hii (ya jana Jumanne)."

Amewapongeza wanajeshi 150,000 wa kike na kiume ambao wamewahi kuhudumu huko Afghanistan katika kipindi cha karibu miongo miwili iliyopita, huku akiwaenzi waliouawa katika mstari wa mbele. Amesema, "katu hamtosahaulika."

Kwa mujibu wa jeshi la Ujerumani, ni askari 59 tu wa kijerumani waliouawa nchini Afghanistan tokea mwaka 2001.

Huku hayo yakijiri, katika hali ambayo mchakato wa kuondoka wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan umeshika kasi kabla ya Septemba 11 kama alivyoahidi Rais Joe Biden, lakini vyanzo vya habari vimedokeza kuwa, Washington inataka kutia ulimi puani tena.

Marekani inasuasua kuwaondoa wanajeshi wake vamizi Afghanistan

Duru za habari zinaarifu kuwa, huenda wanajeshi elfu moja Marekani wakabaki nchini Afghanistan eti kwa ajili ya kulinda ubalozi wa US mjini Kabul na Uwanja wa Ndege mjini hapo.

Wadadisi wa mambo wanasema kuwa, uwepo wa askari wa Marekani na wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO haujawa na matunda yoyote ghairi ya mauaji dhidi ya raia, kushadidi ukosefu wa usalama na kuongezeka pakubwa uzalishaji na magendo ya mihadarati nchini Afghanistan.