-
Russia: Marekani ilifanya kosa la kistratijia kujiondoa JCPOA
May 09, 2020 23:42Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kuwa viongozi wa Marekani hawana uwezo wa kuandaa mazingira ya kurefushwa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.
-
Utafiti: Wamarekani 150,000 katika hatari ya kujiua kutokana athari za janga la corona
May 09, 2020 08:09Utafiti mpya unaonyesha kuwa huenda makumi ya maelfu ya wananchi wa Marekani wataaga dunia kwa kunywa pombe kupita kiasi, kubugia dozi zilizopitiliza za mihadarati au kujiua kutoka na msongo wa mawazo uliosababishwa na janga la corona.
-
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaitaka Marekani ihitimishe hatua zake za upande mmoja
May 08, 2020 07:04Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inapaswa kuhitimisha hatua zake za upande mmoja na zenye madhila.
-
Spika Nancy Pelosi: Njaa na umasikini vinaitesa Marekani
May 08, 2020 06:59Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani amekiri kwamba, baada ya virusi vya Corona kuenea nchini humo, hivi sasa nchi hiyo inakabiliwa na ongezeko kubwa la umasikini na njaa.
-
Marekani yaondoa nchini Saudia mifumo yake ya makombora ya Patriot
May 08, 2020 03:47Marekani imeanza kuondoa katika ardhi ya Saudi Arabia mifumo yake ya makombora ya Patriot na zana zingine za kijeshi, ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kupunguza uungaji mkono wake wa kijeshi kwa utawala huo wa kifalme.
-
Kuongezeka pakubwa ukosefu wa usalama wa chakula Marekani kufuatia kuenea virusi vya Corona
May 07, 2020 21:53Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na kitivo kimoja nchini Marekani, sambamba na kuenea virusi vya Corona na kuibuka mgogoro wa kiuchumi, uhaba mkubwa wa usalama wa chakula katika familia nyingi za Marekani umepanda zaidi.
-
Biden: Si sahihi kuiruhusu Israel iuteke Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
May 07, 2020 08:47Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats amesema kuwa, si sahihi kuiruhusu Israel iuteke Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuuingiza katika ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni zilizopachikwa jina bandia la Israel.
-
Corona yasababisha zaidi ya watu milioni 20 kupoteza ajira nchini Marekani
May 07, 2020 08:27Zaidi ya watu milioni 20 wamepoteza ajira kikamilifu nchini Marekani kutokana na janga la corona.
-
Amnesty: Marekani imepunguza idadi ya raia iliyowaua katika operesheni za kijeshi
May 07, 2020 03:16Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limetofautiana na idadi iliyotangazwa na Washington ya raia waliouawa katika operesheni za kijeshi za Marekani mwaka jana 2019 katika nchi mbali mbali duniani.
-
Rouhani: Iran haitakubali ukiukwaji wa azimio 2231
May 06, 2020 06:46Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Tehran katu haitakubali ukiukwaji wowote wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ameongeza kuwa: "Ni haki isiyopingika ya Iran kuwa, vikwazo vya silaha viondolewe dhidi yake hivi karibuni katika fremu ya azimio hilo."