Amnesty: Marekani imepunguza idadi ya raia iliyowaua katika operesheni za kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60824-amnesty_marekani_imepunguza_idadi_ya_raia_iliyowaua_katika_operesheni_za_kijeshi
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limetofautiana na idadi iliyotangazwa na Washington ya raia waliouawa katika operesheni za kijeshi za Marekani mwaka jana 2019 katika nchi mbali mbali duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2020 03:16 UTC
  • Amnesty: Marekani imepunguza idadi ya raia iliyowaua katika operesheni za kijeshi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limetofautiana na idadi iliyotangazwa na Washington ya raia waliouawa katika operesheni za kijeshi za Marekani mwaka jana 2019 katika nchi mbali mbali duniani.

Daphne Eviatar, Mkurugenzi wa Usalama wa HRW amesema "kwa mujibu wa maeneo ambayo tumeyafanyia uchunguzi wa kina, jeshi la Marekani lingali linapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya raia waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi yake."

Kwa mujibu wa shirika hilo lenye makao makuu yake mjini New York, mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani yaliua raia wasio na hatia kati ya 416 na 1,030 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka jana 2019 katika nchi ya Syria pekee. Amnesty imesema raia zaidi ya 15 waliuawa katika hujuma hizo za anga za jeshi la Marekani nchini Somalia mwaka jana.

Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya US (Pentagon) imehalalisha mauaji hayo kwa kudai kuwa: "Ingawaje mauaji ya raia na kitu kisichoepukika katika vita, lakini Jeshi la Marekani linajitahidi kupunguza maafa hayo ya raia."

Aghalabu ya mauaji ya raia yanayofanywa na US ni kupitia hujuma za drone

Hii ni katika hali ambayo, takwimu mpya zilizotolewa na Pentagon jana Jumatano zinadai kuwa, raia 130 pekee ndio waliouawa katika operesheni za kijeshi za Marekani mwaka jana katika nchi za Iraq, Syria, Afghanistan na Somalia.

Pentagon imesema jeshi la Marekani mwaka jana 2019 liliua raia 108 nchini Afghanistan, 22 katika nchi za Iraq na Syria na raia wawili pekee nchini Somalia.