-
Raia wa Malaysia waanzisha kampeni ya kupinga vikwazo na vitisho vya Marekani dhidi ya Iran
May 30, 2019 00:01Makundi kadhaa ya wananchi kwa kushirikiana na wanaharakati wa kijamii na kisiasa nchini Malaysia yameanzisha kampeni ya kupinga vitisho na vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kadhalika ngoma ya vita ya Washington katika eneo la Asia Masgharibi.
-
Hizbullah: Mashinikizo kuulenga muqawama daima hayatokuwa na natija yoyote
May 29, 2019 23:27Kaimu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba Marekani na Israel kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za eneo la Asia Magharibi zinaulenga mrengo wa muqawama kwa mashinikizo makali, amesisitiza kuwa hatua hizo hata kama zitaendelea daima, lakini hazitofikia natija.
-
Papa: Sera ya US ya kutenganisha watoto wa wahajiri na wazazi wao ni ukatili
May 29, 2019 03:46Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameitaja sera ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuwatenganisha watoto wadogo na wazazi wao wahajiri kuwa ni ukatili.
-
Wakazi wa mji wa Hiroshima, Japan wafanya maandamano kulaani majaribio ya Marekani ya silaha za nyuklia
May 28, 2019 23:20Wakazi wa mji wa Hiroshima nchini Japan wamefanya maandamano kulaani majaribio ya hivi karibuni ya silaha za nyuklia yaliyofanywa na Marekani.
-
Kuunga mkono Russia ubunifu wa Iran wa kupunguza hali ya taharuki Ghuba ya Uajemi
May 28, 2019 07:00Ili kufikia malengo yake haramu katika eneo la Asia Magharibi na Ghuba ya Uajemi, Marekani daima imekuwa ikieneza chuki dhidi ya Iran yaani Iranophobia, na kwa njia hiyo imeibua hitilafu na mgogoro katika uhusiano wa Iran na majirani zake katika Ghuba ya Uajemi. Pamoja na hayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo uthabiti katika Ghuba ya Uajemi na hata imewasilisha mpango mpya kuhusiana na hilo.
-
Zarif akimhutubu Trump; Kiongozi Muadhamu ameshatangaza silaha za nyuklia ni haramu
May 27, 2019 23:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumatatu usiku amejibu madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwa eti Iran inafuatilia silaha za nyuklia na kusema, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshatangaza kuwa silaha za nyuklia ni haramu.
-
Iran: Hatufanyi mazungumzo ya moja kwa moja, au yasiyo ya moja kwa moja na Marekani
May 27, 2019 04:03Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amepuuzilia mbali madai yaliyoenea hivi karibuni kwamba Tehran inafanya mazungumzo na Marekani kwa shabaha ya kupunguza taharuki baina ya nchi mbili.
-
Safari ya Trump Japan, Washington kuitumia Tokyo kuanzisha tena mazungumzo na Korea Kaskazini
May 26, 2019 21:51Rais Donald Trump wa Marekani anafanya safari ya siku tatu nchini Japan.
-
Wairaq wafanya maandamano makubwa kulaani siasa za Marekani dhidi ya Iran
May 26, 2019 06:56Maelfu ya raia wa Iraq wamefanya maandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mkoa wa Baghdad na Basra wakilalamikia siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yafanyika Marekani
May 26, 2019 06:31Mamia ya raia wa Marekani wameandamana kupinga ubaguzi wa rangi unaotekelezwa na kundi la wazungu wenye misimamo ya kufurutu ada katika jimbo la Ohio, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.