Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yafanyika Marekani
Mamia ya raia wa Marekani wameandamana kupinga ubaguzi wa rangi unaotekelezwa na kundi la wazungu wenye misimamo ya kufurutu ada katika jimbo la Ohio, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Maandamano hayo ya wapinzani wa ubaguzi yalijiri baada ya kufanyika mkutano wa wanaharakati wa kundi la wazungu wa kundi la kibaguzi la Ku Klux Klan ambao wanaamini kuwa wazungu ndio kaumu bora zaidi ya wanadamu wote.
Wafuasia wa harakati inayopinga ubaguzi waliandamana Jumamosi katika jimbo la Ohio na kuvuruga mjumuiko huo wa wabaguzi wa rangi wenye misimamo ya kuufurutu ada.
Wanaopinga ubaguzi walifanikiwa kuwazuia wafuasi hao wa kundi la kibaguzi la Ku Klux Klan kutoa hotuba zao.
Rais Donald Trump wa Marekani ambaye analaumiwa kuwa mbaguzi mkubwa wa rangi amekataa kulaani harakati za uvunjaji sheria za makundi ya wazungu wabaguzi kama Ku Klux Klan.
Mwananadharia na mhadhiri mashuhuri wa taaluma ya siasa katika Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana alisema kuwa Doland Trump, ndiye rais mbaguzi zaidi wa rangi katika historia ya nchi hiyo.
Francis Fukuyama alisema kuwa Trump anawachochea wabaguzi wa rangi wa mrengo wa kushoto kuendelea kuwa na misimamo ya kupindukia mipaka na ya ubaguzi dhidi ya jamii nyingine za nchi hiyo. Fukuyama amesema hatua hizo za Trump ni za makusudi kwa sababu hataki kuwa na mpinzani mwenye nguvu katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.