Hizbullah: Mashinikizo kuulenga muqawama daima hayatokuwa na natija yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53794-hizbullah_mashinikizo_kuulenga_muqawama_daima_hayatokuwa_na_natija_yoyote
Kaimu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba Marekani na Israel kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za eneo la Asia Magharibi zinaulenga mrengo wa muqawama kwa mashinikizo makali, amesisitiza kuwa hatua hizo hata kama zitaendelea daima, lakini hazitofikia natija.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2019 23:27 UTC
  • Hizbullah: Mashinikizo kuulenga muqawama daima hayatokuwa na natija yoyote

Kaimu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba Marekani na Israel kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za eneo la Asia Magharibi zinaulenga mrengo wa muqawama kwa mashinikizo makali, amesisitiza kuwa hatua hizo hata kama zitaendelea daima, lakini hazitofikia natija.

Sheikh Ali Da'mush amesema kuwa lengo la vikwazo, mzingiro na mashinikizo dhidi ya mrengo wa muqawama na washirika wa muqawama huo, ni kutaka kuwafanya waachane nao. Kama ambavyo pia Washington na washirika wake wanataka mrengo huo wa muqawama uhitimishe uungaji mkono wake kwa harakati hizo na kwamba kamwe jambo hilo halitofanikiwa. Sheikh Da'mush amezidi kufafanua kwamba wapenzi wa muqawama hii leo wamesimama imara kuliko wakati mwingine wowote ule katika kuunga mkono muqawama kwa kuwa harakati hiyo ni chanzo na msingi wa nguvu ya Lebanon katika kukabiliana na tamaa na vitisho vya utawala haramu wa Kizayuni.

Sheikh Da'mush, Kaimu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah

Amesema kuwa lau kama si muqawama basi Israel ingekuwa inafanya mashambulizi yake ya kila siku nchini Lebanon. Kabla ya hapo pia Sayyid Hashim Safi Al Din, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah sambamba na kuashiria mzingiro wa kichuki unaofanywa na nchi kadhaa zenye kupenda kujitanua kuulenga muqawama alisema kuwa, lengo la mzingiro huo ni kuzidisha mashinikizo kwa watu wote ambao wanashirikiana na muqawama ili hatimaye waweze kuacha ushirikiano huo. Hata hivyo amesema kuwa kinyume na matarajio ya adui njama za maadui hao zimekuwa zikienda kinyume na malengo yao kwani muqawama umekuwa imara zaidi mwaka huu wa 2019 kuliko hata miaka miwili iliyopita.