-
Marekani yapanua kisiri uwepo wake wa kijeshi Tunisia
Sep 24, 2018 22:54Ripoti mpya imefichua kuwa Marekani imekuwa ikipanua kisiri uwepo wake wa kijeshi nchini Tunisia, licha ya upinzani kusisitiza kuwa kitendo hicho ni uingiliaji wa masuala ya ndani na kukanyaga uhuru wa kujitawala nchi hiyo.
-
Iran: Ndoto ya Marekani ya kuzuia uuzwaji mafuta ya nchi hii, haina tafsiri
Sep 24, 2018 10:49Waziri wa Mafuta wa Iran sambamba na kubainisha kwamba mbali na Korea Kusini, hakuna nchi iliyocha kununua mafuta ya nchi hii na kusisitiza kuwa, ndoto ya Marekani ya kusimamisha kabisa uuzaji nje mafuta ya Iran haitathibiti.
-
Wanafunzi wenye asili ya Afrika wazidi kunyanyaswa na polisi wa Marekani
Sep 23, 2018 23:27Matokeo ya uchunguzi uliosambazwa hivi karibuni kabisa unaonesha kuongezeka ukandamizaji na unyanyasaji wa polisi wa Marekani dhidi ya wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari wenye asili ya Afrika katika mji wa Philadelphia.
-
Iran yalalamikia ripoti mpya ya Marekani kuhusu ugaidi
Sep 23, 2018 12:30Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, madai yaliyomo kwenye ripoti ya kila mwaka ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu ugaidi ni ya kinafiki kama ilivyokuwa kwa ripoti zote za kila mwaka za wizara hiyo.
-
Hamas: Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kikwazo katika kuboreka hali ya mambo Ghaza
Sep 23, 2018 10:32Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kikwazo kikuu katika kuboreka hali ya mambo ya Ukanda wa Ghaza.
-
Marekani imewatorosha viongozi wa DAESH (ISIS) eneo la Deir ez-Zor, Syria
Sep 22, 2018 23:11Duru za kuaminika za Syria zimetangaza kuwa muungano wa kijeshi wa kimataifa unaoongozwa na Marekani wa eti kupambana na DAESH (ISIS) umewatorosha viongozi kadhaa wa kundi hilo la kigaidi na ukufurishaji katika eneo la Deir ez-Zor mashariki mwa Syria.
-
Trump anajiandaa kukutana na Kim Jong-un, huku Russia ikiikosoa Marekani
Sep 22, 2018 23:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kuwa, Rais wa nchi hiyo Donald Trump anajiandaa kwa mkutano wa pili na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini.
-
Iran yakanusha madai ya kuomba kufanya mazungumzo na Trump
Sep 21, 2018 23:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja kama kichekesho madai kwamba taifa hili limeomba kufanya mkutano na Rais Donald Trump wa Marekani.
-
Wabunge wa Kisuni Iraq: Marekani inatushinikiza tumteue tena Haider al-Abadi kuwa Waziri Mkuu
Sep 20, 2018 10:53Mjumbe wa Mrengo wa Ujenzi wa Iraq ambaye pia ni mbunge wa Kisuni katika Bunge la nchi hiyo amefichua kuwa serikali ya Marekani inawashinikiza wabunge wote wa Kisuni nchini Iraq wamuungE mkono Haider al-Abadi ili ateuliwe tena kuwa waziri mkuu.
-
Marekani: Tupo tayari kuanza upya mazungumza na Korea Kaskazini
Sep 20, 2018 10:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa, nchi yake imejiandaa kuanza haraka mazungumzo ya kutokomeza silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na kwamba mazungumzo hayo yatakamilika ifikapo mwezi Januari 2021.