Marekani yapanua kisiri uwepo wake wa kijeshi Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48369-marekani_yapanua_kisiri_uwepo_wake_wa_kijeshi_tunisia
Ripoti mpya imefichua kuwa Marekani imekuwa ikipanua kisiri uwepo wake wa kijeshi nchini Tunisia, licha ya upinzani kusisitiza kuwa kitendo hicho ni uingiliaji wa masuala ya ndani na kukanyaga uhuru wa kujitawala nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 25, 2018 02:24 UTC
  • Marekani yapanua kisiri uwepo wake wa kijeshi Tunisia

Ripoti mpya imefichua kuwa Marekani imekuwa ikipanua kisiri uwepo wake wa kijeshi nchini Tunisia, licha ya upinzani kusisitiza kuwa kitendo hicho ni uingiliaji wa masuala ya ndani na kukanyaga uhuru wa kujitawala nchi hiyo.

Jarida la The National Interest limenukuu ripoti ya tovuti ya habari ya Task & Purpose inayoendeshwa na maveterani wa kijeshi ikisema kuwa, kikosi cha Marine Corps Raiders cha jeshi la Marekani kilishiriki pakubwa katika operesheni ya kijeshi dhidi ya magaidi mwaka 2017, kikishirikiana na jeshi la serikali katika nchi moja ya kaskazini mwa Afrika.

Jarida hilo limenukuu vyanzo vya habari ndani ya Kamandi ya Jeshi la Marekani Afrika AFRICOM vikisema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba operesheni hiyo ya kukabiliana na genge la kigaidi lenye mfungamano na mtandao wa al-Qaeda ilifanyika nchini Tunisia.

Marekani imekuwa ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi nchini Tunisia tokeo mwaka 2014, ilipotuma makumi ya askari wa Kikosi cha Operesheni Maalumu katika mpaka wa magharibi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mpaka wa magharibi wa Tunisia

Japokuwa askari wa Marekani wamekuwepo kwa miaka mingi katika nchi mbalimbali za Afrika lakini idadi ya akari hao imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika nchi za bara hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Vilevile Marekani inaendelea kujenga na kupanua vituo vya kijeshi katika nchi za Afrika kwa visingizo mbalimbali.