Baraza la Usalama lalaani hatua ya US kumteka nyara Maduro
Wawakilishi wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiwemo waitifaki wa Marekani, wamelaani kitendo cha Washington cha kumteka nyara Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura kujadili uvamizi huo wa Marekani dhidi ya Venezuela na kutekwa nyara kwa Rais Maduro. Mabalozi wa Marekani na Venezuela walishambuliana kwa maneno makali katika kikao hicho, huku Katibu Mkuu wa UN akieleza wasiwasi wake kuhusu mustakabali wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini.
Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, amesema: Kukamatwa kwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na Marekani kunatishia kuirudisha dunia katika enzi ya "machafuko na dhuluma." Shambulio la Washington dhidi ya taifa la Amerika Kusini limeonyesha nidhamu ya dunia ambayo Marekani inataka kuweka, mwanadiplomasia huyo alikiambia kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Jumatatu, akiongeza kuwa "linawatisha hata wale wanaopinga Atlantiki kwa dhati."
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeed Iravani amesema kutekwa nyara kwa Rais aliyechaguliwa na wananchi na mke wake ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kanuni zinazohusiana na kinga na utu wa watu waliopewa wakuu wa nchi na serikali kwa mujibu wa sheria za kimataifa, na inachukuliwa kuwa shambulio kubwa dhidi ya kanuni ya usawa wa uhuru wa nchi.
Katika barua iliyotumwa kwa Baraza la Usalama siku ya Jumamosi, Balozi wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa, Samuel Reinaldo Moncada Acosta alilaani shambulio hilo la Marekani na kulitaka baraza hilo kuchukua hatua za haraka dhidi ya Washington. Mjumbe huyo alionya kwamba, kutokana na mashambulizi hayo, Venezuela ina "haki yake ya asili ya kujilinda" chini ya sheria za kimataifa.