Wanafunzi wenye asili ya Afrika wazidi kunyanyaswa na polisi wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48345-wanafunzi_wenye_asili_ya_afrika_wazidi_kunyanyaswa_na_polisi_wa_marekani
Matokeo ya uchunguzi uliosambazwa hivi karibuni kabisa unaonesha kuongezeka ukandamizaji na unyanyasaji wa polisi wa Marekani dhidi ya wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari wenye asili ya Afrika katika mji wa Philadelphia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 24, 2018 02:57 UTC
  • Wanafunzi wenye asili ya Afrika wazidi kunyanyaswa na polisi wa Marekani

Matokeo ya uchunguzi uliosambazwa hivi karibuni kabisa unaonesha kuongezeka ukandamizaji na unyanyasaji wa polisi wa Marekani dhidi ya wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari wenye asili ya Afrika katika mji wa Philadelphia.

Televisheni ya al Jazeera ya lugha ya Kiingereza imewanukuu wanaharakati wa masuala ya kijamii wa Marekani wakisema kuwa, uonevu na unyanyasaji dhidi ya wanafunzi wenye asili ya Afrika umeongezeka sana katika mji wa Philadelphia wa jimbo la Pennsylvania la kaskazini mashariki mwa Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanafunzi wenye asili ya Afrika katika mji wa Philadelphia wako katika hatari ya kudhalilishwa na polisi kwa mara tatu zaidi ikilinganishwa na wanafunzi wengine.

Polisi wa Marekani wakimkandamiza mtu mwenye asili ya Afrika

 

Wanaharakati wa haki za kijamii wameongeza kuwa, ni kutokana na ukandamizaji na unyanyasaji huo ndio maana wanafunzi wengi wa shule za msingi na sekondari wenye asili ya Afrika huishia kufungwa jela.

Televisheni hiyo imeongeza kuwa, idadi kubwa ya wanafunzi wasio wazungu hufungwa jela kwa tuhuma za kufanya fujo na hupitisha umri wao wa ujana wakiwa gerezani.

Vitendo vya kibaguzi na unyanyasaji wa polisi wa Marekani dhidi ya wananchi wenye asili ya Afrika vimeongezeka sana baada ya kuingia madarakani Donald Trump, rais mbaguzi wa rangi huko Marekani.