Amnesty International: Israel inafanya "maangamizi ya kizazi" katika Ukingo wa Magharibi
-
Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi wakilazimishwa kuhama makazi yao
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekutaja kuongezeka vitendo vya ukatili vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi kuwa ni "maangamizi ya kizazi" na "kulazimisha watu kuhama makazi yao."
Shirika la Amnesty International, likinukuu takwimu za karibuni, limetangaza kwamba kati ya Januari 2023 na Aprili 2026, nyumba 117 za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi zilibomolewa kabisa au kwa sehemu, na wakazi wa nyumba hizo wamelazimika kuondoka katika nyumba zao. Uhamishaji huu wa kulazimishwa umefikisha idadi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao hadi takriban 5,910 katika kipindi hicho.
Amnesty International pia imesisitiza kwamba katika kipindi hicho hicho, vituo vipya 363 vya makazi haramu ya walowezi vilianzishwa na utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi, huku nyumba na miundombinu 3,407 ya Wapalestina ikibomolewa.
Shirika hilo la haki za binadamu limezitaja hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni sehemu ya "sera iliyopangwa" ya kuimarisha uvamizi na kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiziayuni katika Ukingo wa Magharibi, likizitaja kuwa ni risasi ya mwisho dhidi ya haki ya uhuru na usalama wa Wapalestina wanaopishi katika eneo hilo.