-
Maandamano ya Wapalestina mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani
Sep 05, 2018 22:25Idadi kubwa ya Wapalestina wamefanya maandamano mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wakilalamikia hatua ya serikali ya Washington ya kukata misaada yake kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa Ajili ya Wapalestina (UNRWA).
-
Ayatullah Jannati: Kujiondoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya Iran liwe funzo
Sep 04, 2018 09:02Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ahamad Jannati ameashiria Marekani kuvunja ahadi zake na kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran, JCPOA, na kusema hilo linapaswa kuwa funzo kuhusu mazungumzo na Marekani.
-
Hizbullah: Marekani haina ubavu wa kuwawekea masharti walioshinda vita Syria
Sep 04, 2018 03:37Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa Marekani ambayo sera zake za kuyasaidia makundi ya kigaidi kwa ajili ya kuindoa madarakani serikali halali ya Syria zimefeli na kushindwa haina haki na ubavu wa kutoa masharti ya kuondoka washauri wa kijeshi wa Iran na wapiganaji wa Hizbullah nchini Syria ambao wameshinda vita dhidi ya magaidi.
-
Kuongezeka uwezekano wa kujiuzulu Waziri wa Ulinzi wa Marekani
Sep 03, 2018 22:08Suala la uwezekano wa kujiuzulu James Mattis, Waziri wa Ulinzi wa Marekani limeendelea kupata nguvu kutokana na kushtadi tofauti katika ikulu ya Marekani (White House).
-
Canada yaunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran na kuondoa utegemezi kwa sarafu ya dola ya Marekani
Sep 03, 2018 22:04Maamuzi ya upande mmoja ya kisiasa na kimabavu ya Marekani katika kipindi cha utawala wa rais Donald Trump yanaendelea kukabiliwa na upinzani kote duniani.
-
Hizbullah: Kukombolewa Idlib kutapiku turufu ya mwisho ya Marekani, Israel na Saudia nchini Syria
Sep 03, 2018 03:24Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema, kukombolewa mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria ambayo ni ngome ya mwisho ya magaidi katika nchi hiyo litakuwa pigo kubwa kwa Magharibi, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia.
-
Maneva makubwa ya kijeshi ya Russia Bahari ya Mediterranean, majibu kwa vitisho vinavyozidi kuongezeka vya Marekani dhidi ya Syria
Sep 02, 2018 01:26Ushindi mkubwa linaoendelea kuupata jeshi la Syria na waitifaki wake katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, na hatua ya jeshi hilo ya kujiandaa hivi sasa kuusafisha mkoa wa Idlib kutokana na uchafu wa magenge ya kigaidi, imewatia kiwewe waungaji mkono wa magaidi hao yaani nchi za Magharibi na hasa Marekani. Mkoa wa Idlib ndiyo ngome ya mwisho wa magenge ya kigaidi nchini Syria.
-
Radiamali ya Wapalestina baada ya kukatwa kikamilifu misaada ya Marekani kwa UNRWA
Sep 01, 2018 21:48Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka kuchukuliwa hatua kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na njama za Washington dhidi ya Palestina. Hiyo ni baada ya Marekani kuchukua uamuzi wa kukata kikamilifu misaada yake ya kifedha kwa Shirika la Umoja wa Mataifa Linalotoa Misaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina.
-
Katibu Mkuu wa UN akosoa vikali uamuzi wa Marekani wa kukata misaada yake kwa UNRWA
Sep 01, 2018 09:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na shirika la umoja huo la ufikishaji misaada na uandaaji ajira kwa ajili ya wakimbizi Wapalestina UNRWA wamelaani uamuzi wa Marekani wa kukata misaada yake kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.
-
Kuendelea kupingwa uingiliaji wa Marekani katika mchakato wa kuundwa serikali mpya nchini Iraq
Aug 31, 2018 02:01Kongresi ya Taifa ya Iraq imesisitiza kuwa, uingilkiaji wa Marekani katika suala la kuundwa serikali mpya ya nchi hiyo umezidi kuvuruga hali ya kisiasa na kuzidi kuufanya tata mwenendo wa kisiasa wa Iraq.