Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umewatia nguvuni na kuwaweka kizuizini makumi ya Wanamfalme na mawaziri wa zamani na wa sasa wa utawala huo kwa kisingizio cha kupambana na ufisadi.
Duru za polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimearifu kuwa watu karibu 30 wametiwa nguvuni katika maandamano dhidi ya serikali katika mji wa Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu ya Kaskazini huko mashariki mwa nchi hiyo.
Polisi ya utawala wa Aal Khalifa unaendelea kukabiliana kwa njia mbalimbali na wanaharakati wa kisiasa huko Bahrain huku wapinzani nchini humo wakiendelea kila uchao kuwekwa jela kwa visingizio visivyo na msingi.
Maafisa wa kulinda usalama nchini Algeria wamewatia mbaroni watu sita wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kuwa, imewatia mbaroni watu 12 wakiwemo madaktari na wauguzi kadhaa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya magendo ya viungo vya binadamu.
Mkuu wa Taasisi ya Kisheria na Demokrasia (BIRD) nchini Bahrain, Ahmad al Wadai ametangaza kuwa, utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa umemhamishia jela Zainab Marhun mwanaharakati wa kisiasa wa nchi hiyo.
Mahakama ya Malawi imetoa kibali cha kukamatwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Joyce Banda kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka yake wakati alipokuwa kiongozi wa nchi hiyo.
Askari wa utawala wa Kizayuni wa israel wamewavamia Wapalestina waliofanya mgomo wa kukaa kitako katika msikiti wa Al-Aqsa na kuwatia nguvuni zaidi ya watu mia moja.
Mkuu wa masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru kutoka kwenye magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel ametangaza kuwa watoto 1,200 Wapalestina hutiwa nguvuni kila mwaka na askari wa utawala huo haramu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Mtafiti wa Kiirani wa masuala ya kensa aliyekamatwa hivi karibuni mara tu baada ya kuwasili Marekani ameachiliwa huru na kurudishwa humu nchini.