Dec 30, 2017 07:37 UTC
  • Makumi ya wapinzani watiwa mbaroni Equatorial Guinea

Chama kimoja cha upinzani cha Equatorial Guinea kimesema kuwa, makumi ya wanachama wake wametiwa mbaroni na serikali.

Bonifacio Angema, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha Citizens for the Innovation cha Equatorial Guinea amesema kuwa, askari wa serikali juzi Alkhamisi walivamia majengo ya ofisi za chama hicho katika miji ya Malabo na Bata, miji mikuu ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo na kuwatia mbaroni makumi ya wafuasi wa chama hicho.

Bendera ya Equatorial Guinea

 

Angema amewalaumu vikali polisi wa serikali kwa kuwakandamiza wafuasi wa chama chake na kuwajeruhi vibaya kiasi kwamba baadhi ya wanachama wa chama hicho wamelazwa hospitalini.

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Citizens for the Innovation cha Equatorial Guinea amesema, wafuasi wa chama hicho wametiwa mbaroni na maafisa wa serikali muda mchache baada ya kufanyika uchaguzi mkuu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za kuthibitisha au kukanusha habari hiyo kutoka upande wa serikali ya Equatorial Guinea.

Tags