Apr 29, 2024 02:36 UTC

Polisi nchini Marekani imemtia nguvuni mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini humo ambaye alikuwa katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Washington.

Jill Stein, mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini Marekani ambaye alikuwa amejumuika katika maandamano ya waungaji mkono wa Palestina katika Chuo Kikuu cha Washington na kisha kutiwa nguvuni na polisi  aliandika jana katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba, polisi wa nchi hiyo pia wamewakamata Jason Cole, mkurugenzi wa kampeni za uchaguzi na naibu wake, Kelly Merrill Kair. 

Bi Stein ameeleza kuwa hawataondoka mahali hapo hadi vyuo vikuu vya Marekani visusie taasisi na vituo vya kitaaluma vya utawala wa Israel.

Maandamano yanayoendelea kufanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Kizayuni yaliyoanzia katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York nchini  Marekani, sasa yamesambaa katika vyuo vikuu vingine vya nchi hiyo vikiwemo vyuo vikuu vya Yale, New York, Harvard, Texas na Southern California.  Maandamano wa wanafunzi wa vyuo vikuu kupinga mauaji ya Israel huko Palestina pia tayari yamefika katika vyuo vikuu vya nchi nyingine za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Canada, Uingereza na Australia. 

Tags