Jan 06, 2018 16:41 UTC
  • Wanawafalme wengine 11 walioandamana dhidi ya Bin Salman Riyadh watiwa mbaroni

Wanawafalme 11 walioandamana mbele ya kasri la ufalme wa Saudi Arabia mjini Riyadh wametiwa mbaroni na askari wa gadi ya mfalme wa nchi hiyo na kupelekwa jela ya al-Ha'ir ya nchi hiyo.

Wanawafalme hao ambao waliamua kuandamana mbele ya kasri la mfalme kulalamikia maamuzi ya serikali ya Riyadh ya kufuta msamaha kwa wanamfalme wa kulipa gharama za maji na umeme wametiwa mbaroni na askari wa kitengo cha 'al-Seif al-Ajrab' wa gadi ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud. Kwa mujibu wa duru za ndani ya serikali nchini Saudia, wanawafalme hao pia waliandamana mbele ya kasri la mfalme wakitaka kulipwa fidia kufuatia kutolewa hukumu ya kisasi kwa mmoja wa ndugu yao.

Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa Saudia

Hii ni katika hali ambayo, Jamal Khashoggi mwandishi mashuhuri wa Saudia katika mtandao wa kijamii wa Twitter sambamba na kuashiria ongezeko la wimbi jipya la kamatakamata dhidi ya wanawafalme lililoanza tarehe nne Januari mwaka huu 2018 amesema, kamatakamata hiyo inatokana na hatua ya wanawafalme hao kukosoa utendajikazi mbovu wa serikali kuhusiana na baadhi ya masuala. Itafaa kuashiria kuwa, tangu alipochukua hatamu za uongozi Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa Saudia, amekuwa akitekeleza siasa za kuwashusha hadhi wanawafalme wengine ili kwa njia hiyo aweze kumaliza kambi ya upinzani dhidi yake.

Polisi wa Saudia

Kwa mujibu wa duru za habari nchini humo, Bin Salman amekusudia pia kuwavua sifa ya 'Uanawafalme' ili kuufanya ukoo wa Aal-Saud kuwa mdogo. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni na kwa kisingizio cha kupambana na ufisadi, Mohammad Bin Salman aliwaweka kizuizini wanawafalme kadhaa wa ukoo huo wa kifalme nchini Saudia.

Tags