-
IOM: Zaidi ya wahajiri 1000 wamekufa mwaka huu katika Bahari ya Mediterania
Jul 02, 2018 14:01Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) limetangaza kuwa, zaidi ya wahajiri 1000 wamefariki dunia katika Bahari ya Mediterania tangu ulipoanza mwaka huu wa 2018.
-
Maelfu ya Wamarekani waandamana dhidi ya sera za Trump kuhusu wahajiri
Jul 01, 2018 01:43Maelfu ya watu wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya Marekani wakipinga sera na siasa za kuwapiga vita wahajiri hususan hatua ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ya kuwatenganisha watoto wahajiri na wazazi wao.
-
Mahakama ya Virginia: Marufuku mpya ya usafiri ya Trump ni ya kibaguzi na inakiuka katiba
Feb 16, 2018 07:42Mahakama ya Jimbo la Virginia nchini Marekani imeitaja marufuku mpya ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo inayowazuia raia wa baadhi ya nchi kuingia Marekani, kuwa inawabagua Waislamu.
-
CARE: Watu milioni 70 duniani wanakabiliwa na migogoro iliyotelekezwa
Jan 23, 2018 07:49Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la CARE International limesema zaidi ya watu milioni 70 wamenasa katika migogoro iliyotelezwa na kupuuzwa kote duniani.
-
Mgogoro mkubwa wa Congo DR ndio uliopuuzwa zaidi mwaka 2017
Dec 20, 2017 03:43Uchunguzi wa maoni uliofanywa na mashirika ya misaada ya kibinadamu umebaini kuwa, mgogoro mkubwa wa kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio uliopuuzwa zaidi katika mwaka huu unaomalizika wa 2017.
-
Viongozi wa nchi saba za Afrika na Ulaya wachunguza mwenendo wa uhajiri nchini Ufaransa
Aug 29, 2017 04:24Viongozi wa nchi saba za Kiafrika na Ulaya wamekutana nchini Ufaransa kwa ajili ya kuchunguza namna ya kupunguza wimbi la uhajiri kutoka nchi za Afrika kuelekea barani Ulaya.
-
Algeria: Mitandao ya magendo ya binaadamu inatishia usalama wa nchi zote za Afrika
Jul 11, 2017 08:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema kuwa, mitandao ya magendo ya binaadamu inatishia usalama na amani ya nchi zote duniani.
-
Morocco: Afrika ichukue hatua shirikishi kukabiliana na wimbi la uhajiri
Jul 04, 2017 07:47Mfalme Mohammed VI wa Morocco imetoa mwito kuzitaka nchi za Afrika kuchukua hatua ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la uhajiri.
-
Kuundwa kundi shirikishi kwa ajili ya kupambana na wahajiri haramu
Mar 16, 2017 04:16Serikali za Uhispania, Ufaransa na Niger zimeunda muungano wa pamoja kwa ajili ya kupambana ipasavyo na kadhia ya wahajiri haramu na magendo ya binaadamu.
-
Raia zaidi ya milioni mbili wa Sudan Kusini wakimbilia nchi jirani
Jan 10, 2017 02:50Raia wengi wa Sudan Kusini wamelazimika kuihama nchi hiyo na kukimbilia katika nchi jirani kutokana na mgogoro wa kisiasa na mauaji yanayoendelea nchini humo.