-
Mapigano yanaendelea Myanmar, hofu ya maelfu ya Warohingya kuzingirwa
Jun 18, 2024 02:34Kundi la kabila lenye silaha nchini Myanmar linajiandaa kufanya mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi katika mji wa pwani kwenye mpaka na Bangladesh, huku kukiwa na hofu kwamba makumi ya maelfu ya Waislamu wa Rohingya watakamatwa katika mapigano magharibi mwa nchi hiyo.
-
UN: Migogoro mingine isifanye wakimbizi Warohingya wasahaulike
Oct 18, 2023 03:51Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa isishugulishwe tu na migogoro mipya na kuwasahau wakimbizi Waislamu Warohingya wa Myanmar.
-
Helikopta na ndege kivita za jeshi la Myanmar zashambulia na kuua makumi ya watu
Apr 11, 2023 11:51Jeshi la Myanmar limefanya mashambulizi ya anga katika mji wa kati mwa nchi hiyo unaojulikana kuwa ngome ya upinzani dhidi ya mapinduzi yaliyofanywa na jeshi hilo miaka miwili iliyopita.
-
Umoja wa Mataifa wasikitishwa na hatua ya kufutwa vyama 40 vya upinzani nchini Myanmar
Mar 31, 2023 11:22Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa na ripoti iliyotolewa ikieleza kuwa, tume ya uchaguzi ya Myanmar iliyoteuliwa na jeshi la nchi hiyo imevifuta vyama 40 vya upinzani, kikiwemo chama cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi.
-
Umoja wa Mataifa waomba misaada kwa ajili wakimbizi wa Rohingya
Dec 28, 2022 08:01Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limeziomba msaada kwa nchi mbalimbali kwa ajili ya wakimbizi wa Rohingya baada ya Waislamu wasiopungua 20 wa jamii hiyo kuaga dunia baharini na mamia ya wengine kunusurika kifo katika ufuo wa Indonesia baada ya wiki kadhaa za kutangatanga katika Bahari ya Hindi.
-
UN yataka dunia iwasaidie wakimbizi Waislamu wa Rohingya
Aug 26, 2022 07:25Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuwasaidia kwa hali na mali wakimbizi Waislamu wa Rohingya walioko nchini Bangladesh.
-
UN yalishutumu jeshi la Myanmar kwa kutenda jinai za vita, mauaji na utesaji
Mar 16, 2022 07:33Umoja wa Mataifa umesema, jeshi la Myanmar limehusika na ukiukaji wa kimpangilio wa haki za binadamu ambao umefikia kiwango cha jinai za vita na jinai dhidi ya binadamu.
-
UN yaitaka jamii ya kimataifa izidi kulishinikiza jeshi Myanmar likomeshe ukatili
Jan 29, 2022 08:05Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameitaka jamii ya kimataifa izidishe mashinikizo kwa jeshi la Myanmar ili likomeshe kampeni yake ya ukatili na ukandamizaji dhidi ya watu wa Myanmar na kusisitiza kurejeshwa mara moja utawala wa kiraia nchini humo.
-
Kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela Aung San Suu Kyi
Dec 08, 2021 02:33Mahakama nchini Myanmar imemhukumu kifungo cha miaka minne jela Aung San Suu Kyi kiongozi wa kilichokuwa chama tawala nchini humo cha National League for Democracy (NLD).
-
Baraza la Usalama lataka kuhitimishwa ukandamizaji dhidi ya raia nchini Myanmar
Nov 12, 2021 02:23Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa inayoelezea wasiwasi mkubwa kuhusu machafuko yanayoendelea nchini Myanmar, ambapo wanajeshi waliotwaa madaraka ya nchi wanafanya ukandamizaji dhidi ya wapinzani na kutoa wito wa kuhitimishwa vitendo hivyo.