-
Mfalme wa Jordan akataa kukutana na Netanyahu na hata kuzungumza naye kwa simu
Aug 04, 2019 03:42Mfalme Abdallah II wa Jordan amekataa ombi la Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel la kukutana naye na hata kufanya naye mazungumzo kwa njia ya simu.
-
Trump na Netanyahu wabwabwaja baada ya Iran kuongeza urutubishaji wa urani
Jul 08, 2019 02:22Hatua ya Iran ya kuingia kwenye awamu ya pili ya kupunguza kiwango cha ahadi zake ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa mujibu wa kifungu nambari 36 cha mapatano hayo, imewatia kiwewe Rais Donald Trump wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Mike Pompeo.
-
Netanyahu apata pigo la kihistoria, uchaguzi mpya waitishwa Israel
May 30, 2019 06:57Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, limepiga kura ya kujivunja baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya mseto na hivyo kulazimika kuitisha uchaguzi mpya.
-
Msemaji wa Netanyahu ashambuliwa vikali kwa kuwaita waandamanaji wa Kipalestina 'wake za ISIS'
Mar 31, 2019 03:19Msemaji wa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu amejiwa juu na watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuwaita wanawake wa Kipalestina walioshiriki maandamano ya 'Haki ya Kurejea' huku wakiwa wamevalia vazi la stara la niqabu kuwa eti ni wake za wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS (Daesh).
-
Netanyahu atoa vitisho dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza, Qassam nayo yajibu vitisho hivyo
Mar 29, 2019 03:50Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametoa vitisho dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ambao umekuwa ukizingirwa mwa miaka mingi sasa, na kudai kuwa Israel itashadidisha mashambulizi ya kinyama katika eneo hilo.
-
Jihadul Islami yawaonya Wazayuni wasithubutu kushambulia Ghaza
Mar 25, 2019 09:05Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel usithubutu kufanya shambulio lolote dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
-
Vyama vya mrengo wa kulia Israel vinapanga kumuangusha Netanyahu
Dec 31, 2018 06:51Baada ya kusambaratika baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel na kuchukuliwa uamuzi wa kufanyika uchaguzi wa bunge wa kabla ya wakati katika utawala huo, vyama vya mrengo wa kulia katika muungano tawala vimekumbwa na mgawanyiko mkubwa na sasa vinafuatilia mpango wa kumuangusha waziri mkuu Benjamin Netanyahu.
-
Zarif amshangaa Netanyahu kwa kusifia makombora mapya ya Israel
Dec 18, 2018 12:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali kitendo cha Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel cha kuonesha majivuno na kusifia makombora mapya ya utawala huo wa Kizayuni.
-
Mawaziri sita wa serikali ya Israel washiriki katika maandamano ya kupinga serikali
Dec 17, 2018 11:50Baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanamapambano wa Palestina na kulazimika Israel kukomesha uvamizi wake wa Ghaza baada ya siku mbili tu, sasa hivi utawala wa Kizayuni umekumbwa na maandamano ya kuipinga serikali huku mawaziri sita wa serikali hiyo nayo wakishiriki kwenye maandamano ya jana usiku ya kumpinga waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
-
Ripoti: 70% ya kauli za viongozi wa Israel wakiongozwa na Netanyahu, ni porojo
Nov 20, 2018 04:31Utafiti mpya umefichua kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya matamshi yanayotolewa na wanasiasa wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni urongo, porojo na propaganda, huku Waziri Mkuu wa utawala huo pandikizi, Benjamin Netanyahu akiongoza katika orodha hiyo.