Netanyahu asalimu amri, akiri kushindwa kuunda serikali
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56778-netanyahu_asalimu_amri_akiri_kushindwa_kuunda_serikali
Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekiri kuwa ameshindwa kuunda serikali ya muungano, baada ya mazungumzo ya kisiasa kati yake na mshindani wake mkuu katika uchaguzi uliopita wa bunge, Benny Gantz kugonga mwamba.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 22, 2019 04:32 UTC
  • Netanyahu asalimu amri, akiri kushindwa kuunda serikali

Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekiri kuwa ameshindwa kuunda serikali ya muungano, baada ya mazungumzo ya kisiasa kati yake na mshindani wake mkuu katika uchaguzi uliopita wa bunge, Benny Gantz kugonga mwamba.

Hapo jana Ofisi ya Rais Reuven Rivlin wa utawala huo wa KIzayuni ilitangaza kuwa, Netanyahu amerejesha jukumu la kuunda serikali katika ofisi hiyo na sasa Benny Gantz wa muungano wa Blu na Nyeupe (yaani Blue and White Alliance) anatazamiwa kupewa jukumu hilo.

Binafsi amekuwa akisisitiza kuwa, iwapo Netanyahu anataka serikali ya muungano, sharti yeye (Gantz) awe Waziri Mkuu. Gantz atakuwa na siku 28 pekee za kufanya majadiliano ya kuunda serikali hiyo ya muungano, vinginevyo matokeo ya uchaguzi huo yatafutiliwa mbali.

Benny Gantz wa muungano wa Blu na Nyeupe

Katika uchaguzi wa pili wa bunge la utawala wa Kizayuni katika kipindi cha miezi sita ya hivi karibuni uliofanyika Septemba 17, chama cha Likud cha Netanyahu kilipoteza viti vingi.

Chama cha Likud kilipata viti 55, huku muungano wa Blu na Nyeupe (yaani Blue and White Alliance) wa Gantz ukipata viti 54, suala ambalo linaonyesha kuwa mirengo yote miwili imezidi kuporomoka.