Netanyahu apata pigo la kihistoria, uchaguzi mpya waitishwa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53809-netanyahu_apata_pigo_la_kihistoria_uchaguzi_mpya_waitishwa_israel
Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, limepiga kura ya kujivunja baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya mseto na hivyo kulazimika kuitisha uchaguzi mpya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2019 06:57 UTC
  • Netanyahu apata pigo la kihistoria, uchaguzi mpya waitishwa Israel

Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, limepiga kura ya kujivunja baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya mseto na hivyo kulazimika kuitisha uchaguzi mpya.

Siku ya Jumatano Knesset, ilipiga kura ya kujivunja na hivyo kuandaa uchaguzi mpya ambao umepangwa kufanyika mwezi wa Septemba.

Netanyahu alishinda uchaguzi wa Aprili baada ya chama chake cha mrengo wa kulia cha Likud kushinda viti 35 kati ya 120 na alitakiwa kuunda serikali ya mseto kufikia Jumatano. Alishindwa kufanya hivyo hata baada ya kufanya mazungumzo na muitifaki wake Avigdor Lieberman. Imearifiwa kuwa Netanyahu alishindwa kufikia maufaka na vyama venye misimamo mikali ya kidini.

Netanyahu amepata pigo kubwa kwani hii ndio mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa utawala huo ghasibu kushindwa kuunda serikali ya mseto na kulazimisha bunge kuitisha uchaguzi wa mapema.

Hayo yanajiri wakati ambao Netanyahu anakabiliwa na kashfa kadhaa za ufisadi na hivyo anapingwa vikali na vyama vya mrengo wa kulia na kulikuwa na tetesi kuwa amefika mwisho wa maisha yake ya kisiasa.

Bunge la utawala bandia wa Israel, Knesset

Pamoja na hayo, Rais Trump wa Marekani amekuwa akiunga mkono hatua zilizo kinyume cha sheria za Netanyahu ikiwa ni pamoja na kuutambua utawala wa Kizayuni wa Israel kama mmiliki wa Miinuko ya Golan ya Syria. Aidha kufuatia uchochezi wa Netanyahu, Trump amelitangaza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran kuwa eti ni kundi la kigaidi. Hatu hizo zilichukuliwa ili kumsaidia Netanyahu kushinda uchaguzi. 

Netanahu amepata pigo hilo huku Wapalestina na wapenda uhuru duniani wakijitayarisha katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kesho Ijumaa kwa lengo la kulaani jinai za utawala haramu wa Israel na kuunga mkono harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.