-
Serikali ya Nigeria yaufungia mtandao wa Twitter kwa muda usiojulikana
Jun 05, 2021 07:12Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, hatua ya mtandao wa kijamii wa Twitter ya kuufuta ujumbe mmoja wa Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo haikubaliki kabisa hivyo Abuja ameamua kuufungia mtandao huo kwa muda usiojulikana. Twitter kwa upande wake imesema inafuatilia kwa kina suala hilo.
-
Jeshi la Nigeria laangamiza magaidi 50 wa Boko Haram
Jun 03, 2021 22:15Jeshi la Nigeria limetangaza habari ya kuangamiza magaidi wasiopungua 50 wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.
-
Familia za wanafunzi waliotekwa nyara Nigeria zaitaka serikali kuwakomboa
Jun 02, 2021 07:02Familia za wanafunzi waliotekwa nyara na magenge ya wahalifu nchini Nigeria na vilevile jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu zimeitaka serikali ya Nigeria kuchukua hatua madhubuti za kukomboa karibu wanafunzi 200 wa shule moja ya Kiislamu waliotekwa nyara na magenge ya wahalifu katikati mwa Nigeria.
-
Kuendelea harakati za magaidi nchini Nigeria; wanafunzi 200 watekwa nyara
Jun 01, 2021 21:58Makundi ya kigaidi katika eneo la Afrika Magharibi hasa nchini Nigeria yamekithirisha vitendo vya uhalifu, na katika tukio la hivi karibuni wanafunzi karibu 200 wa shule moja ya Kiislamu wametekwa nyara kati mwa Nigeria.
-
Wanamgambo 10 wa Boko Haram waangamizwa na jeshi la Nigeria
Jun 01, 2021 03:47Wanamgambo 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Nigeria.
-
Makumi watoweka baada ya boti kuzama mtoni nchini Nigeria
May 27, 2021 02:55Makumi ya watu hawajulikana waliko baada ya boti iliyokuwa imejaza abiria kupindukia kuzama katika mto mmoja huko kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Kamanda wa Majeshi ya Nigeria Ibrahim Attahiru afariki dunia katika ajali ya ndege
May 22, 2021 12:01Mkuu wa Majeshi ya Nigeria Luteni Jenerali Ibrahim Attahiru, amepoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokkea katika jimbo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo la Kaduna.
-
Mkuu wa genge la Boko Haram ajipiga risasi kutaka kujiua Nigeria
May 22, 2021 02:05Serikali na jeshi la Nigeria limethibitisha habari zinasosema kuwa, Abubakar Shekau, mkuu wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram amejipiga risasi begani katika jaribio la kutaka kujiua. Hii ni katika hali ambayo vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa, Shekau amejiua.
-
Wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria washiriki matembezi ya Siku ya Quds
May 08, 2021 07:51Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana Ijumaa walijitokeza kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mikubwa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Bunge la Nigeria lataka kushughulikiwa tatizo la ukosefu wa usalama unaoikabili nchi
Apr 29, 2021 03:35Bunge la Nigeria limepasisha maazimio kadhaa yanayomtaka Rais wa nchi, vikosi vya ulinzi na jeshi la polisi nchini humo kushughulikia tatizo la ukosefu wa usalama katika baadhi ya majimbo ya nchi hiyo ambalo limekuwa likiyatesa maeneo hayo kwa miaka kadhaa sasa.