-
Afisa wa UN aitaka Israel imwachie huru Maher al Akhras haraka iwezekanavyo
Oct 25, 2020 23:03Ripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel ameutaka utawala wa Kizayuni umwachie Mpalestina Maher al Akhras haraka iwezekanavyo.
-
Al Houthi: Kuna udharura wa kuwa na msimamo mmoja dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw)
Oct 25, 2020 13:14Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen amesema kuna udharura wa kuwepo msimamo mmoja wa Kiislamu dhidi ya vitendo vya kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu.
-
Harakati za mapambano Palestina zaapa kulipiza kisasi cha mauaji ya kijana Amer
Oct 25, 2020 09:19Harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zimetangaza kuwa zitajibu mauaji yaliyofaywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 18 wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi kwa kuzidisha mapambano dhidi ya utawala huo.
-
Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu walaani makubaliano kati ya Sudan na Israel
Oct 24, 2020 04:15Nchi za ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu pamoja na makundi ya muqawama yamelaani vikali hatua ya kufikiwa makubaliano kati ya Sudan na Israel ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina yao. Wananchi wa Palestina wamekitaja kitendo hicho cha kisaliti kama 'dhambi ya kisiasa.'
-
Hamas: Israel haiwezi kuvunja azma na mapambano ya Wapalestina
Oct 24, 2020 00:50Msemaji wa Harakati ya Mapambabno ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa lengo la mashambulizi ya mara kwa mara ua utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza ni kuvunja azma ya mapambano ya taifa la Palestina lakini utawala huo utashindwa na kugonga mwamba.
-
Jordan yasisitiza tena kuundwa nchi huru ya Palestina
Oct 19, 2020 23:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan ametaka ipatikane amani ya kweli na kiuadilifu itakayodhamini kuundwa nchi huru ya Palestina.
-
Watu wa Palestina wakusanyika kumuunga mkono mateka Maher al-Akhras
Oct 16, 2020 10:15Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wamekusanyika leo kutangaza kumuunga mkono Maher Al Akhras, mateka Mpalestina anayeshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
EU yaikosoa Israel kwa kuendelea kupora ardhi za Wapalestina
Oct 16, 2020 04:12Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amekosoa uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Hamas: Imarati na Bahran ziipe Israel baadhi ya ardhi zao....
Oct 15, 2020 07:57Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza kuwa kama watawala wa Imarati na Bahrain wanaliona suala la kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel ni jambo la kawaida basi watoe baadhi ya ardhi za nchi zao kwa utawala huo haramu.
-
Imarati yasema Wapalestina hawana shukrani kwa kukosoa uhusiano na Israel
Oct 15, 2020 04:38Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu amewashutumu vikali wananchi wa Palestina na kudai kuwa hawana shukrani wala hawatambui fadhila, kutokana na hatua yao ya kupinga hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.