Watu wa Palestina wakusanyika kumuunga mkono mateka Maher al-Akhras
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64054-watu_wa_palestina_wakusanyika_kumuunga_mkono_mateka_maher_al_akhras
Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wamekusanyika leo kutangaza kumuunga mkono Maher Al Akhras, mateka Mpalestina anayeshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 16, 2020 10:15 UTC
  • Maher al-Akhras
    Maher al-Akhras

Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wamekusanyika leo kutangaza kumuunga mkono Maher Al Akhras, mateka Mpalestina anayeshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Maher Al Akhras ni mateka Mpalestina ambayo amesusia chakula kwa muda wa siku 82 mfululizo akilalamikia kushikiliwa kwa muda katika jela ya utawala wa Kizayuni wa Israe.

Khidhr Habib, mwanachama wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amewahutubia watu waliokuwa wamekusanyika kumuunga mkono al-Akhras mbele ya ofisi za Shirika la Kimataifa la Hilaly Nyekundu na Msalaba Mwekundi mjini Ghaza na kusema Al Akhras ni mtetezi wa uadilifu na matukufu ya kidini na dunia inapaswa kudiriki ni dhulma gani inayotendewa taifa la Palestina.

Hali ngumu na isiyo ya kibinadamu ya magereza ya Israel imepelekea mateka kadhaa kususia chakula kama njia ya kubainisha malalamiko yao.

Jela ya Israel

 

Kwa kuzingatia hali hiyo, mateka 30 wa Kipalestina katika gereza ya Ofer, ambao ni wanachama wa Harakati ya Jihad Islami, Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, wameamua kususia chakula katika kuwaunga mkono Maher al Akhras.

Karibu mateka 4,800 wa Palestina wakiwemo wanawake 41 na watoto 140 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel. Mateka hao wa Palestina ni kati ya waathirika wakubwa wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.