-
Ismail Haniya: Historia haitawahurumia walioanzisha uhusiano na utawala wa Israel
Oct 13, 2020 08:12Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema historia haitazihurumia hata kidogo nchi za Kiarabu kutokana na hatua ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na mataifa nayo hayatasahau kitendo hicho.
-
Palestina katika njia ya umoja na mshikamano wa ndani
Oct 12, 2020 23:09Baada ya baadhi ya nchi za Kiarabu kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kulitelekeza waziwazi taifa la Palestina, sasa hivi makundi ya Palestina yameelewa kuwa njia pekee ya kulinda uwepo wa taifa lao ni umoja na mshikamano.
-
Matusi ya gazeti la Okaz la Saudi Arabia dhidi ya Wapalestina, ni zaidi ya kuvunja mwiko
Oct 11, 2020 07:51Gazeti la Saudi Arabia la Okaz limewatukana Wapalestina na harakati za mapambano za taifa hilo likisema kuwa ni "maadui wa Saudia".
-
Tahadhari kuhusu njama ya Wazyuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa
Oct 11, 2020 04:37Sheikh Ekrima Sa'id Sabri, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) na khatibu katika Msikiti wa Al Aqsa mjini humo ametahadharisha kuhusu njama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kutaka kutwaa sehemu ya msikiti huo ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Gazeti la Saudia lawatukana Wapalestina, ladai ni maadui wa Waarabu
Oct 11, 2020 00:45Gazeti la Okaz la Saudi Arabia limewatukana wananchi na makundi ya muqawama ya Palestina na kudai ni maadui wa Saudia.
-
Israel yaingiwa na kiwewe kuhusu kuanza Intifadha mpya Palestina
Oct 10, 2020 08:46Mkuu wa Idara ya Utafiti katika Shirika la Ujasusi katika Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel (AMAN) amebainisha wasi wasi wake kuhusu kuanza Intifadha au mwamko mpya wa Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
-
EU yaishurutisha Palestina kulipa kodi kwa Israel ili iendelee kuisaidia kifedha
Oct 08, 2020 10:35Umoja wa Ulaya umesema utaipatia Palestina msaada wa fedha kwa sharti la kulipa kodi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Uenyekiti wa Arab League wageuka kiazi moto, Libya pia yaukataa
Oct 07, 2020 04:23Siku chache baada ya Qatar na Kuwait kukataa kuchukua uenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) badala ya Palestina ambayo nayo ilikataa uenyekiti huo, Libya pia imeamua kufuata mkumbo huo.
-
Mwanamfalme wa Saudia akerwa na Palestina kupinga uhusiano na Israel
Oct 07, 2020 01:16Mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi ya Saudi Arabia amewakosoa vikali viongozi wa Palestina kwa kupinga hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Hamas: Waandishi wa habari wasiupe jukwaa utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 06, 2020 04:13Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewakosoa waandishi wa habari hususan katika nchi za Kiarabu kwa kumpa waziri wa vita wa Israel jukwaa la kuhubiri siasa na sera za utawala huo haramu.