Gazeti la Saudia lawatukana Wapalestina, ladai ni maadui wa Waarabu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63943-gazeti_la_saudia_lawatukana_wapalestina_ladai_ni_maadui_wa_waarabu
Gazeti la Okaz la Saudi Arabia limewatukana wananchi na makundi ya muqawama ya Palestina na kudai ni maadui wa Saudia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2020 00:45 UTC
  • Gazeti la Saudia lawatukana Wapalestina, ladai ni maadui wa Waarabu

Gazeti la Okaz la Saudi Arabia limewatukana wananchi na makundi ya muqawama ya Palestina na kudai ni maadui wa Saudia.

Gazeti hilo limeandika makala nzima ya kuwatukana Wapalestina. Katika sehemu moja ya makala hiyo, mwandishi Muhammad al Said wa Saudi Arabia amedai kuwa, wananchi wa Palestina wametuma magaidi katika nchi nyingi za Kiarabu na silaha na mabomu ili kuwaua Waarabu.

Lakini pia viongozi wa Saudi Arabia kwa miaka mingi wamekuwa wakichukua misimamo ya uadui wa waziwazi dhidi ya taifa la Palestina linalokandamizwa kila upande na Wazayuni. Mfano wa wazi kabisa ni matamshi ya Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia aliyoyatoa mwezi Machi 2017 nchini Marekani. 

Ushirikiano wa Saudi Arabia na Wazayuni dhidi ya Waislamu na Waarabu ni wa muda mrefu sana

 

Akihojiwa na jarida la Kimarekani la Atlantic, Bin Salman alisema, Saudia ina manufaa mengi na Israel, na kama amani itapatikana basi kutapatikana manufaa makubwa baina ya Israel na wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi pamoja na nchi kama Misri na Jordan. Kwa kweli kwa matamshi yake hayo, mrithi huyo wa kiti cha ufalme cha Saudi Arabia ni kama alitangaza rasmi kuutambua utawala wa Kizayuni wa Israel.

Vile vile si ajabu hata kidogo gazeti la Okaz la Saudia kuwatukana wananchi wa Palestina kwani Riyadh ni muungaji mkono mkubwa wa njama za Marekani za "Muamala wa Karne" ambazo lengo lake hasa ni kuiangamiza kikamilifu kadhia ya Palestina na kuisahaulisha kabisa.