Israel yaingiwa na kiwewe kuhusu kuanza Intifadha mpya Palestina
Mkuu wa Idara ya Utafiti katika Shirika la Ujasusi katika Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel (AMAN) amebainisha wasi wasi wake kuhusu kuanza Intifadha au mwamko mpya wa Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain baada ya kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu; tarehe 15 mwezi Septemba mwaka huu zilisaini huko White mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala huo wa Kizayuni. Tukio hilo lilihudhuriwa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Dror Shalom ameyasema hayo leo katika mahojiano na gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth na kuongeza kuwa: "Uwezekano wa kusambaratika serikali ya Mamlka ya Ndani ya Palestina na kuanza Intifadha mpya ni jambo linaloitia wasi wasi Israel."
Shaleom ameongeza kuwa, kadhia ya Palestina ni kama bomu linalokaribia kulipuka.
Baada ya kuwasilisha mpango wa Kizayuni-Kimarekani wa 'Muamala wa Karne' pamoja na mpango wa kupora zaidi ardhi za Palestina katika Ukingo wa Magharibi sambamba na hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, Wapalestina wametangaza azma ya kuimarisha mapambano na muqawama kukabiliana na njama hizo sambamba na kutosalimu amri.

Aidha tarehe 28 Januari, Rais Donald Trump wa Marekani akiwa pamoja na waziri mkuu wa utawala bandia wa Israel, Benjamin Netanyahu alizindua mpango wa ubaguzi wa Muamala wa Karne.
Kuitambua rasmi Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, kuupatia utawala huo haramu umiliki wa asilimia 30 ya eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, kupingwa haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea nchini kwao na kupokonywa silaha kikamilifu itakayoitwa nchi ya Palestina ni miongoni mwa vipengele vya mpango huo wa udhalilishaji.