-
Jinai ya kutisha; Israel yaua shahidi Wapalestina 150 Gaza
Jul 13, 2025 02:02Wapalestina zaidi ya 150 wameuawa shahidi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, huku eneo hilo la pwani likishuhudia siku yake mbaya zaidi tangu mwezi Mei, wakati utawala wa Israel uliposhadidisha mauaji yake ya kimbari dhidi ya eneo hilo.
-
Wabunge 60 wa UK waitaka London ilitambue taifa la Palestina
Jul 12, 2025 12:50Kufuatia mpango tata wa Israel wa kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Gaza na kuwapeleka Rafah, takriban wabunge 60 wa Uingereza wameitaka serikali ya London kulitambua rasmi taifa la Palestina.
-
Raia wa US apigwa hadi kufa na walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi
Jul 12, 2025 09:41Walowezi wa Israel wamempiga hadi kufa kijana mmoja raia wa Marekani katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, kwa mujibu wa familia yake na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
-
Uhispania na Ireland kujiunga na nchi zaidi ya 20 zitakazochukua 'hatua madhubuti' dhidi ya Israel
Jul 11, 2025 13:15Uhispania na Ireland zitajiunga na zaidi ya nchi 20 zitazokutana katika mji mkuu wa Colombia, Bogota wiki ijayo kutangaza "hatua madhubuti" dhidi ya ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Upeo wa ukatili; Israel yaua Wapalestina zaidi ya 80 Gaza ndani ya saa 24
Jul 10, 2025 23:24Mashambulizi ya Israel katika maeneo mbali mbali huko Gaza yameua shahidi watu wasiopungua 82 tangu alfajiri ya jana, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea ya kusitisha mapigano hayo.
-
Unajua kwa nini Marekani imemuwekea vikwazo Ripota Maalumu wa UN kuhusu Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu?
Jul 10, 2025 22:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alitangaza Jumatano, Julai 9, kwamba atamuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu, kwa kile alichokiita "juhudi zisizo halali zinazohusiana na uchunguzi wake kuhusu vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza" na eti kwa kuchukua "hatua dhidi ya maafisa wa Marekani na Israel."
-
Al-Qassam yamwangamiza askari wa Kizayuni baada ya kutofanikiwa kumkamata mateka
Jul 10, 2025 09:40Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS limetangaza kuwa limelazimika kumuangamiza mwanajeshi mmoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza baada ya mazingira kwenye medani ya mapambano kutoruhusu kumkamata mateka.
-
HAMAS: Ghaza haitasalimu amri; Muqawama ndio utakaotoa masharti
Jul 10, 2025 04:05Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS Izzat al-Rishq amesema, Ghaza haitasalimu amri, na ni Muqawama ndio utakaotoa masharti, si utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kwa nini njama za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimeshindwa licha ya kuzingirwa Gaza?
Jul 08, 2025 23:05Licha ya kuendelea mzingiro wa Gaza na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina, lakini makundi ya muqawama ya Palestina yanaendelea kusimama kidete na kukabiliana na njama za Wazayuni.
-
Jeshi la Israel lakiri askari wake 5 wameangamizwa, 14 wamejeruhiwa Ghaza
Jul 08, 2025 08:52Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limetangaza kuwa askari wake watano wameuawa na wengine 14 wamejeruhiwa katika mapigano kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.