-
Jordan kumuita balozi wake wa Romania kupinga hatua ya nchi hiyo dhidi ya Quds
Apr 17, 2019 23:29Jordan imesema kuwa itamuita nyumbani balozi wake wa Romania, ikiwa ni jibu kwa hatua ya nchi hiyo ya Ulaya kutangaza kuwa itauhamishia ubalozi wake katika mji wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kutoka Tel Aviv.
-
Rais wa Lebanon: Tangazo la Trump kuhusu miinuko ya Golan na Quds ni kinyume na maazimo ya kimataifa
Apr 11, 2019 23:55Rais Michel Aoun wa Lebanon kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, tangazo la Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na umiliki wa utawala vamizi wa Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria linakinzana na maazimio ya kimataifa.
-
Rouhani: Quds ni mji mkuu wa kudumu wa Palestina na Golan haiwezi kutenganishwa na Syria
Apr 06, 2019 21:58Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Quds ni mji mkuu wa kudumu wa Palestina na miinuko ya Golan ni ardhi ya Syria isiyotenganishika na ardhi nyingine za nchi hiyo na kwamba hatua yoyote iliyo kinyume na hivyo ni kukanyaga maamuzi wa Umoja wa Mataifa na ni kinyume na uhakika wa kihistoria.
-
Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa kaskazini mwa Quds imeongezeka
Mar 18, 2019 10:56Vyombo vya habari vya Kizayuni leo Jumatatu vimetangaza kuwa kuhani mmoja wa Kizayuni ambaye alijeruhiwa katika oparesheni ya kijana wa Kipalestina karibu na kitongoji cha Ariel kaskazinii mwa mji wa Salfit katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan ameaga dunia.
-
Matakwa matatu ya Kamisheni ya Masuala ya Palestina ya Bunge la Jordan dhidi ya Israel
Mar 15, 2019 03:51Kamisheni ya Masuala ya Palestina ya Bunge la Jordan imetoa wito wa kufukuzwa balozi wa Israel mjini Amman, kurejeshwa nyumbani balozi wa Jordan huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kufutwa mkataba wa gesi na Israel.
-
Spika wa Bunge la Lebanon: Eneo lote la Quds ni mji mkuu wa Palestina
Mar 11, 2019 23:24Spika wa Bunge la Lebanon kwa mara nyingine tena amesisitiza msimamo wa nchi yake kuhusiana na kuiunga mkono Baytul -Muqaddas na Palestina na kusema kuwa, eneo lote la Quds Tukufu ni mji mkuu wa nchi ya Palestina.
-
Wazayuni wawatia nguvuni wasimamizi wa Matukufu ya Kiislamu Quds
Feb 24, 2019 10:49Polisi ya utawala haramu wa Israel imewakamata wasimamizi wa ngazi za juu wa Matukufu ya Kiislamu katika mji mtukufu wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
UN yapinga vikali mashambulizi ya Wazayuni wa Israel huko Quds
Jan 28, 2019 04:06Nickolay Mladinov ambaye ni mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya kijiji cha kaskazini mwa Quds (Jerusalem) hayakubaliki na yanashtua sana.
-
Utawala wa Kizayuni unapanga njama ya kuzima sauti ya adhana Baitul Muqaddas Mashariki
Jan 02, 2019 23:41Televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa manispaa ya utawala huo haramu katika eneo la Baitul Muqaddas Mashariki (East Jerusalem) ina mpango wa kuzuia sauti ya adhana isisikike katika misikiti ya eneo hilo la Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Abbas: Palestina haitaruhusu Marekani iiuzie Israel Quds Tukufu
Jan 01, 2019 04:47Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema Wapalestina katu hawataruhusu Marekani iuuze mji mtukufu wa Quds kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, akisisitiza kuwa mji huo unaokaliwa kwa mabavu ni mji mkuu wa daima wa taifa la Palestina.