Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa kaskazini mwa Quds imeongezeka
Vyombo vya habari vya Kizayuni leo Jumatatu vimetangaza kuwa kuhani mmoja wa Kizayuni ambaye alijeruhiwa katika oparesheni ya kijana wa Kipalestina karibu na kitongoji cha Ariel kaskazinii mwa mji wa Salfit katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan ameaga dunia.
Wanajeshi wawili wa Israel na mlowezi mmoja wa Kiyahudi waliuawa jana kwa kupigwa risasi na kijana wa Kipalestina mwenye miaka 23 karibu na kitongoji cha Wazayuni cha Ariel kaskazini mwa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu. Katika operesheni hiyo wanajeshi kadhaa wa Kizayuni walijeruhiwa. Kijana huyo wa Kipalestina aliyetekeleza oparesheni hiyo dhidi ya wanajeshi wa Kizayuni baadaye alikimbia baada ya oparesheni hiyo ya kimuqawama.
Utawala wa Kizayuni umeimarisha hatua za kiusalama katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan baada ya kupata kipigo hicho; na hadi sasa umeshawatia mbaroni raia kadhaa wa Kipalestina katika eneo hilo. Duru za Palestina zimearifu kuwa makumi ya wanajeshi wa Kizayuni wamekivamia kitongoji cha al Zawiya huko Salfit na kumtia nguvuni Amin Yusuf Abu Laila baba wa kijana wa Kipalestina aliyewauwa askari wa Kizayuni pamoja na mtoto wake mmoja wa kiume.