-
Sayyid Hassan Nasrullah: Ni ujinga wa hali ya juu kuiamini Marekani
May 14, 2018 12:55Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria kitendo cha Marekani cha kuvunja mikataba na maazimio ya kimataifa na kusema kuwa, baada ya tajriba zote ambazo zimeshuhudiwa kwa Washington, ni ujinga wa hali ya juu kuiamini nchi hiyo.
-
Onyo la Hizbullah ya Lebanon kwa Marekani, Israel na Saudi Arabia
May 02, 2018 21:16Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesisitiza kuwa, Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia haziwezi kukaa kimya baada ya kushindwa njama zao katika nchi za Iraq, Syria na Lebanon.
-
Hizbullah: Mashambulizi ya Israel Syria yatawasha moto katika eneo zima
Apr 24, 2018 03:18Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon sambamba na kuielezea kuwa nyeti hali ya hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa, kuendelea mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria si tu kwamba kunahatarisha usalama wa nchi hiyo, bali kuna hatari yatazusha mgogoro katika eneo zima.
-
Mtazamo wa Hassan Nasrullah kuhusiana na uchaguzi wa bunge nchini Lebanon
Apr 11, 2018 02:52Jumapili iliyopita Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon alihutubia eneo la Nabatieh kusini mwa Lebanon ambapo alibainisha maoni yake kuhusiana na uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.
-
Nasrullah: Saudia imependekeza kuipatia Syria mabilioni ya dola ivunje uhusiano wake na Iran
Mar 27, 2018 12:32Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama ya Lebanon Hizbullah amesema utawala wa Aal Saud uliieleza serikali ya Syria kwamba uko tayari kuacha kuyaunga mkono makundi ya kigaidi yanayotenda jinai na kuifisidi nchi hiyo na kuipatia serikali hiyo ya Damascus mamia ya mabilioni ya dola kwa ajili ya kuijenga upya Syria ikiwa nchi hiyo itakuwa tayari kuvunja uhusiano wake na Iran.
-
Indhari ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kwa njama za Marekani
Feb 26, 2018 03:44Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria alipokuwa akihutubia katika mji wa Baalabek juu ya kushindwa mipango ya Marekani na washirika wake katika Mashariki ya Kati na kusambaratishwa kundi la kigaidi la Daesh na kusema kuwa, hii leo tunapaswa kukusanya mafanikio yetu ambapo kubwa zaidi katika hayo ni uungaji mkono unaopata muqawama.
-
Tahadhari ya Sayyid Nasrulah kuhusu njama za Marekani Mashariki ya Kati
Feb 17, 2018 23:42Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa eneo lote la Mashariki ya Kati limekuwa medani ya vita vya mafuta na gesi. Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumzia hitilafu za mpaka wa Lebanon na utawala wa kizayuni wa Israel na mivutano ya pande hizo mbili juu ya vyanzo vya mafuta na gesi katika maji ya pwani ya eneo hilo.
-
Sayyid Nasrullah alipongeza jeshi la Syria kwa kutungua ndege ya kivita ya Israel
Feb 17, 2018 03:56Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amelipongea jeshi la Syria kwa kutungua ndege ya kijeshi aina ya F-16 ya utawala haramu wa Israel na kuitaja hatua hiyo kuwa ni mafanikio makubwa ya kijeshi.
-
Hassan Nasrullah: Inasikitisha kuona bado kuna nchi zinaendeleza uhusiano na Israel
Jan 20, 2018 01:12Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon sambamba na kuzitaka nchi zote za dunia kujiepusha kufanya uhusiano na utawala katili wa Israel, ameonyesha masikitiko kwamba bado kuna nchi zinaendeleza uhusiano na utawala huo.
-
Maandamano dhidi ya Marekani na Israel nchini Lebanon na hotuba muhimu ya Sayyid Hassan Nasrullah
Dec 12, 2017 09:35Maandamano ya kuitetea Beitul-Muqaddas yalifanyika alasiri ya jana katika viunga vya kusini mwa Beirut mji mkuu wa Lebanon na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kisiasa.