-
Iran yaunga mkono kuanza mchakato wa kumtibu kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria
Aug 13, 2019 11:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono mchakato wa kuanza kumpatia matibabu Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kueleza kufurahishwa na hatua ya kuelekea India Sheikh Zakzaky na mkewe kwa ajili ya matibabu.
-
Madaktari wa nchi 7 waiandikia barua serikali ya Nigeria, wataka Sheikh Zakzaky apewe matibabu
Aug 12, 2019 02:44Makumi ya madaktari kutoka nchi 7 duniani wameiandikia barua serikali ya Nigeria wakikumbusha hali mbaya ya kiafya ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky na kutaka apewe matibabu haraka iwezakanavyo.
-
Harakati ya IMN yajibu mapigo, yasema itakabiliana na vizingiti vya serikali ya Abuja
Aug 01, 2019 07:25Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imetangaza kuwa, itabadilisha mbinu zake za kufuatilia suala la kuachiwa huru kiongozi wake anayeendelea kushikiwa korokoroni kwa miaka kadhaa sasa, Sheikh Ibrahim Zakzaky, na kukabiliana na vizingiti na mbinyo wa serikali ya Abuja.
-
Kesi ya Sheikh Zakzaky yaakhirishwa hadi Agosti 5, mawakili wataka aachiwe huru kwa ajili ya matibabu
Jul 29, 2019 12:08Mahakama ya Nigeria leo imeakhirisha kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwa ajili ya kumwachia huru kwa dhamana kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo IMN, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye wafuasi wake wasiopungua 20 waliuawa juma lililopita wakiandamana kwa amani ili kuishinikiza serikali imwachie huru.
-
Mazishi ya wafuasi 6 wa Sheikh Zakzaky waliouliwa shahidi na wanajeshi wa Nigeria yafanyika mjini Abuja
Jul 25, 2019 07:05Shughuli ya kuviaga kwa ajili ya mazishi viwiliwili vya Waislamu sita waliouliwa shahidi katika shambulio la karibuni la wanajeshi wa Nigeria dhidi ya wafuasi wa kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky, ilifanyika jana katika mji mkuu Abuja.
-
Guterres aombwa kufuatilia hali ya Sheikh Zakzaky ili apatiwe matibabu
Jul 25, 2019 02:38Wasomi na wanafikra 52 wamemwandikia barua Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakimtaka asaidie jitihada za kuwaondoa huko Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe Malam Zeenat ili waweze kupatiwa matibabu nje ya nchi haraka iwezekanavyo.
-
Wanachuo wakusanyika mjini Mashhad kumuunga mkono Sheikh Ibrahim Zakzaky
Jul 24, 2019 04:15Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ferdowsi cha mjini Mashhad kaskazini masharikki wa Iran wamefanya mkusanyiko mkubwa na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
-
Wasomi 52 wamtaka Guterres aingilie kati kadhia ya Sheikh Zakzaky
Jul 23, 2019 17:04Wasomi na wanafikra 52 wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asaidie jitihada za kutaka kuachiwa huru mara moja Sheikh Ibrahim Zakzaky huko Nigeria kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
-
Waislamu 6 wafuasi wa Sheikh Zakzaky wauawa kwa kupigwa risasi, Abuja
Jul 23, 2019 04:22Wafuasi 6 wa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wa Nigeria mjini Abuja.
-
Mahakama yaakhirisha kutoa hukumu dhidi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky
Jul 22, 2019 07:59Mahakama Kuu katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria imeakhirisha kutoa hukumu ya kesi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.