-
Rais wa Somalia atangaza janga la njaa kuwa maafa ya taifa
Mar 01, 2017 03:50Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia ametangaza janga la njaa lililoikumba nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kuwa ni maafa ya taifa.
-
WHO: Wasomali zaidi ya milioni moja wanakabiliwa na hatari ya kifo
Mar 01, 2017 00:26Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu uzima na maisha ya zaidi ya Wasomali milioni moja wanaosumbuliwa na baa la njaa.
-
IGAD yaitisha mkutano maalumu kuhusu wakimbizi wa Somalia
Feb 28, 2017 12:52Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za Mashariki mwa Afrika IGAD imeitisha mkutano maalumu mjini Nairobi Machi 25, ili kujadili suluhisho la kudumu la wakimbizi wa Somalia.
-
Mkuu wa shirika la mafuta ateuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Somalia
Feb 23, 2017 10:11Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmaajo aliyeapishwa jana mjini Mogadishu amemteua mkurugenzi wa shirika moja la mafuta kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
-
Rais mpya Somalia aapishwa, aahidi kurejesha heshima ya taifa hilo
Feb 22, 2017 12:38Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo ameapishwa leo mjini Mogadishu katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa nchi kadhaa za kanda hiyo chini ya hatua kali za ulinzi.
-
Sababu ya kuendelea hujuma za kigaidi Somalia
Feb 21, 2017 04:21Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Michael Keating amelaani hujuma ya kigaidi iliyojiri Jumapili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu huku wengi wakihoji sababu ya kuendelea hujuma za kigaidi nchini humo.
-
Atakayetoa taarifa za waliohusika na mlipuko wa Mogadishu kupewa zawadi ya laki moja
Feb 20, 2017 12:31Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ‘Farmajo wa Somalia ametangaza zawadi ya dola laki moja kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kutiwa mbaroni watu waliohusika na shambulio la kigaidi la jana mjini Mogadishu.
-
Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la kigaidi nchini Somalia
Feb 20, 2017 04:34Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Somalia, amelaani shambulizi la kigaidi katika soko moja la Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
39 Wauawa katika hujuma ya kigaidi Mogadishu
Feb 19, 2017 10:41Watu wasiopungua 39 wameuawa leo Jumapili wakati gari lililokuwa limesheheni mabomu liliporipuka katika makutano ya barabara katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Njaa yatishia mamia ya maelfu ya watu nchini Somalia
Feb 16, 2017 12:24Mwakilishi maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametahadharisha kuhusu tishio kubwa la njaa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika na ametoa wito wa kuchukua hatua haraka ili kuzuia maafa ya kibinadamu.